MADIWANI TANGA WAWAFUKUZA KAZI WATUMISHI WANNE

0
1146
Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martin Shigella.
Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martin Shigella.
Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martin Shigella.

NA AMINA OMARI-TANGA

BARAZA la Madiwani la Halmashauri ya Jiji la Tanga limewafukuza kazi watumishi wanne, huku wanane wakishushwa vyeo kwa kudaiwa kukiuka sheria na kanuni za utumishi wa umma, ikiwamo udanganyifu wa kujipatia fedha kwa wananchi.

Akisoma maazimio ya Baraza la Madiwani, Meya wa Jiji la Tanga, Suleiman Mustapha, alisema wamechukuwa hatua hiyo kuhakikisha wanarudisha nidhamu ya utendaji kazi ndani ya jiji hilo.

Alisema miongoni mwa makosa waliyotuhumiwa nayo watendaji hao ni pamoja na matumizi mabaya ya madaraka,  ikiwamo udanganyifu  kwa wananchi wakati wanapotoa huduma.

Aliwataja watumishi waliofukuzwa kazi kuwa ni maofisa ardhi wawili, mwalimu mmoja na mtumishi mmoja wa maabara.

“Mwalimu daraja la tatu, Regina Nestory, mtumishi wa maabara, Femina Kamilisha na Ofisa Ardhi daraja la tatu, Emmanuel Washngton wamefukuzwa kazi kutokana na utoro kazini wakati uhakiki wa vyeti ukiendelea,” alisema Meya Mustapha.

Pamoja na kuchukua uamuzi huo, alisema pia kikao hicho kimeridhia kufukuzwa kazi kwa Ofisa Mtendaji wa Kata ya Kange, Kaombwe Mwanyosi kutokana na kufanya udanganyifu na kujipatia Sh milioni 8 kwa mwananchi, kama mauzo ya kiwanja hali ya kuwa yeye hausiki na uuzaji wa viwanja kwa mujibu wa sheria.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Jiji la Tanga, Daudi Mayeji, aliwataka watumishi kufanya kazi kwa kuzingatia sheria na taratibu za utumishi wa umma katika kuwahudumia wananchi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here