28.3 C
Dar es Salaam
Wednesday, February 21, 2024

Contact us: [email protected]

JAJI KAIJAGE AMRITHI DAMIAN LUBUVA NEC

Jaji wa Mahakama ya Rufaa, Semistocles Kaijage akizungumza na waandishi wa habari.
Jaji wa Mahakama ya Rufaa, Semistocles Kaijage akizungumza na waandishi wa habari.

Na Mwandishi Wetu-DAR ES SALAAM

RAIS Dk. John Magufuli amemteua Jaji wa Mahakama ya Rufaa, Semistocles Kaijage, kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).

Taarifa iliyotolewa jana na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi, ilieza kuwa Jaji Kaijage ameteuliwa kuongoza NEC kwa kipindi cha miaka mitano kuanzia Desemba 20, mwaka huu.

Jaji Kaijage anachukua nafasi ya Jaji mstaafu Damian Lubuva ambaye muda wake wa kuwa mwenyekiti umemalizika rasmi Desemba 19, mwaka huu.

Mbali na hilo, Rais Magufuli pia amemteua Jaji mstaafu Hamid Mahamoud Hamid kuwa Makamu Mwenyekiti wa NEC kwa kipindi kingine cha miaka mitano kuanzia Desemba 20, mwaka huu.

Jaji Hamid alikuwa Makamu Mwenyekiti wa NEC na amemaliza kipindi chake cha kwanza cha miaka mitano, Desemba 19, mwaka huu.

Licha ya uteuzi huo, Rais Magufuli amemteua Jaji mstaafu wa Mahakama ya Rufaa, Harold Nsekela kuwa Kamishna wa Maadili katika Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma kwa kipindi cha miaka mitano kuanzia Desemba 20, mwaka huu.

Katika hatua nyingine, Rais Magufuli amewateua majaji wanne wa Mahakama Kuu kuwa majaji wa Mahakama ya Rufani kuanzia jana.

Majaji hao ni Dk. Gerald Ndika, Jackobs Mwambegele, Rehema Kiwanga na Sivangilwe Mwangesi.

“Wateule wote waliotajwa wataapishwa leo saa 3:00 asubuhi Ikulu, Dar es Salaam,” ilisema taarifa hiyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
583,000SubscribersSubscribe

Latest Articles