23.4 C
Dar es Salaam
Saturday, April 27, 2024

Contact us: [email protected]

KANISA LA EAGT LATOA MIL, 10/- KWA WAATHIRIKA KAGERA

WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa.
WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa.

Na MWANDISHI WETU-DAR ES SALAAM

WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amepokea msaada wa Sh milioni 10 kutoka Kanisa la Evangelistic Assemblies of God Tanzania (EAGT), kwa watu waliothirika na tetemeko la ardhi mkoani Kagera.

Akikabidhi msaada huo, Askofu Mkuu wa EAGT, Dk. Brown Mwakipesile, alisema kanisa limeona lina wajibu wa kuisadia Serikali kuwapunguzia machungu watu waliopatwa na maafa kutokana na tetemeko hilo lililotokea Septemba 10, mwaka huu na kusababisha vifo vya watu 17.

“Tumeona ni vema kanisa la EAGT lishiriki kuisadia Serikali kuwafariji wananchi waliopata maafa kutokana na tetemeko hilo. Tumeona ni wajibu wetu kwa sababu waliopatwa na maafa ni watu wetu wote. Tunawaombea wote waliopatwa na shida waweze kupata nafuu mapema zaidi,” alisema.

Akipokea msaada huo, Waziri Mkuu alisema Serikali itahakikisha michango hiyo inafikishwa kwa walengwa.

“Nawashukuru viongozi wa dini zote kwa jinsi mnavyoisaidia Serikali na mlivyoguswa na kuamua kuwachangia wenzetu waliopatwa na maafa,

“Tunatambua juhudi zinazofanywa na taasisi za dini zote kuunga mkono juhudi za Serikali, tunafarijika mno na tunawashukuru kwa moyo huo,” alisema.

Aidha, alimuomba askofu huyo na viongozi wengine wa dini, kuwaombea viongozi waliopo madarakani ili awape hekima na busara na awawezeshe kuwaongoza vema Watanzania.

Tetemeko hilo la ardhi liliharibu miundombinu ya barabara, shule, zahanati na kujeruhi watu 440, nyumba 2,063 kuanguka huku nyingine 14,081 zikiwa katika hali hatarishi na 9,471 zikipata uharibifu mdogo huku wananchi 126,315 wakihitaji misaada mbalimbali.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles