25.5 C
Dar es Salaam
Friday, September 29, 2023

Contact us: [email protected]

Madiwani Meatu waivunja Mamlaka ya mji mdogo mwhanuzi

Na Derick Milton, Meatu

Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Meatu mkoani Simiyu, wameivunja Mamlaka ya Mji mdogo wa Mwhanuzi ulioko makao makuu ya Wilaya hiyo kwa kile kilichoelezwa ni kushindwa kujiendesha tangu kuanzishwa kwake mwaka 2016.

Uamuzi huo wa kuvunjwa kwa Mamlaka hiyo umefanyika leo Februari 10, kwenye kikao cha Baraza la Madiwani hao, ambacho kilikuwa kikijadili taarifa mbalimbali za robo ya pili ya Halmashauri hiyo.

Kabla ya kufikia uhamuzi wa kuvunjwa kwa Mamlaka hiyo, Madiwani hao wamesema kuwa uendeshwaji wa mmlaka umekuwa mgumu kwani tangu kuanzishwa kwake wameshindwa kukusanya mapato kufikia hata milioni moja.

Wamesema kuwa mbali na kushindwa kukusanya mapato, Mamlaka hiyo imekuwa haina vyanzo vya mapato, huku ikishindwa kujiendesha na badala yake wamekuwa wakitegemea halmashauri kuendesha shughuli zake.

“Ni miaka minne sasa tangu tumeanzisha mamlaka hii lakini hata milioni moja hawajakusanya, imekuwa ni Mamlaka ya kutegemea halmashauri kujiendesha, sasa tumeona huo mzigo hatuuwezi ni bora tukaivunja,” amesema Diwani, Christopher Ndamo.

Diwani kata ya Kimali, Sagika Mahesa, amesema kuwa Mamlaka hiyo imekuwa haina huwezo wa kulipa posho za wajumbe wake kuendesha vikao vyake, kusimamia ofisi, kukusanya mapato na mpaka wapate usaidizi kutoka ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri.

“Halmashauri imekuwa na mambo mengi tumeona kuendelea na Mamlaka ambayo haina huwezo haiwezekani, tunabeba mzigo mkubwa, lakini hii itasaidia shughuli za maendeleo sasa kufanyika kwa urahisi,” amesema Mahesa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,750FollowersFollow
574,000SubscribersSubscribe

Latest Articles