30.8 C
Dar es Salaam
Saturday, February 24, 2024

Contact us: [email protected]

Kunenge aipongeza CRDB kwa kuendelea kupendezesha Tanzania

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Abubakar Kunenge ameipongeza Benki ya CRDB kwa utekelezaji wa mikakati ya kusaidia jitihada za Serikali katika kutunza na kuboresha mazingira.

Kunenge ameyasema hayo leo Februari 10 wakati wa mkutano na watendaji wa mkoa huo ngazi ya kata na mitaa uliofadhiliwa na Benki ya CRDB.

Mkutano huo umefanyika katika ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere uliopo (JNICC) na kuhudhuriwa na watendaji kutoka Wilaya zote za Jiji la Dar es Salaam.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Abubakar Kunenge, akizungumza na watendaji wa kata na mitaa ya Jiji la Dar es Salaam katika Kikao Kazi kilichofanyika katika ukumbi wa JNICC. Kikao hicho kilidhaminiwa na Benki ya CRDB.

Pamoja na mambo mengine mkutano huo umelenga zaidi katika kuhimiza uwajibikaji na utekelezaji wa maagizo ya serikali katika usimamizi wa ukusanyaji wa mapato, usafi wa mazingira, uboreshaji wa miundombinu ya barabara, umeme, maji safi na maji taka ili kutatua kero mbalimbali za wananchi wa Mkoa wa Dar es Salaam.

Kunenge ameishukuru Benki ya CRDB kwa kudhamini mkutano huo huku akiipongeza kwa kampeni ya Pendezesha Tanzania iliyozinduliwa jijini Dar es Salaam mwishoni mwa mwaka 2020 ambayo imelenga kuboresha mwonekano wa mazingira katika maeneo mbalimbali nchini sambamba na upandaji wa miti.

“Nichukue nafasi hii kuwashukuru na kuwapongeza sana Benki ya CRDB kwa kushirikiana kwa karibu na Serikali ya Mkoa wa Dar es Salaam katika kufanikisha mkutano huu ambao moja ya agenda zake ni kujadili namna bora ya kuboresha usafi wa mazingira ya jiji letu la Dar es Salaam,” amesema Kunenge.

Meneja wa Kitengo Wateja Maalumu Benki ya CRDB, Crispin Sichalwe, akitoa mada katika Kikao Kazi cha watendaji wa kata na mitaa ya Jiji la Dar es Salaam. Kikao hicho kilidhaminiwa na Benki ya CRDB.

Pamoja na kugusia suala la usafi wa mazingira, mkuu huyo wa mkoa ameweka mkazo zaidi katika suala la ufanisi wa ukusanyaji mapato huku akiwasisitiza watendaji kusimamia nidhamu ya matumizi ili mapato hayo yakaweze kuonekana na kuleta tija kwa wananchi.

Amesema ukusanyaji wa mapato unapaswa kwenda sambamba na kuboresha mazingira ya biashara ili kuvutia wafanyabiashara.

Sambamba na agenda za kuboresha utendaji, vilevile watendaji wa Serikali ya Mkoa wa Dar es Salaam pia walipata fursa ya kupata elimu ya masuala ya fedha kutoka Benki ya CRDB.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
583,000SubscribersSubscribe

Latest Articles