23.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, June 6, 2023

Contact us: [email protected]

MADIWANI GEITA WAKACHA KIKAO WAKIHOFIA KUKAMATWA

Mkutano kati serikali na Madiwani wa Halmashauri za Mji na Wilaya mkoani Geita, umeshindwa kufanyika kutokana na  madiwani kutofika kwa hofu ya kukamatwa na polisi.

Mkutano huo uliopangwa kufanyika leo Jumatatu Septemba 18, kati ya madiwani hao na Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dk. Mendrad Kalemani na Kamishna wa Madini Mhandisi Benjamin Mchwampaka, kwa ajili ya kujadili mgogoro unaoendelea katika Kampuni ya Uchimbaji Dhahabu ya Geita (GGM), kuhusiana na deni la Dola Milioni 12 ambalo GGM inadaiwa kutolipa kama tozo ya kodi ya huduma.

Mkuu wa Wilaya ya Geita, Herman Kapufi amesema majadiliano hayo yameshindwa kufanyika kwa kuwa wahusika wakuu ambao ni madiwani wengine wako rumande na waliobaki wako mafichoni.

“Kikao kimefanyika bila madiwani na kuhudhuriwa  na wakurugenzi wa halmashauri ambapo kikao kilifikia maazimio baada ya wakurugenzi wa halmashauri zote mbili kukabidhi nyaraka za malalamiko ya madiwani kwa Kamishna wa Madini ili akaoanishe na nyaraka za serikali kwa nia ya kubaini tatizo lilipo,” amesema.

Naye Kamanda wa Polisi wa mkoani Geita, Mponjoli Mwabulambo amesema bado kamata kamata ya madiwani inaendelela na kwamba ambao hawajakamatwa wamekimbia makazi yao kuhofia kukamatwa.

“Kitendo cha mtu kukimbia nyumba yako ni dhahiri kuwa umeshagundua kuwa umetenda kosa lakini kama nilivyosema kuwa uzuri wa sheria ya tuhuma zao zoezi la kuwakamatwa halina ukomo ni bora wajisalimishea kwenye vyombo vya sheria ili kuhojiwa,” amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,303FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles