22.8 C
Dar es Salaam
Saturday, June 3, 2023

Contact us: [email protected]

AJALI YATEKETEZA FAMILIA YA NAIBU WAZIRI, JPM ATUMA RAMBIRAMBI

Familia ya watu 13 ya Naibu Waziri wa zamani wa Viwanda na Biashara, Gregory Teu wamefariki katika ajali iliyotokea  usiku wa kuamkia leo katika barabaraya Masaka, nchini Uganda.

Ajali hiyo imetokea wakati familia hiyo ikiwa njiani kurejea nchini wakitoka katika harusi ya ndugu wa familia hiyo, ambaye ni mtoto wa Teu, nchini Uganda.

Katika basi hilo, kulikuwa na abiria 19 ambapo kati yao waliopona ni sita pekee ambao wamelazwa katika ya Nsambya, nchini Uganda.

Wakati huo huo, Rais John Magufuli ametuma salam za rambirambi kwa Teu, ambaye pia amewahi kuwa Mbunge wa Jimbo la Mpwapwa, mjini Dodoma katika awamu ya nne, kutokana na vifo hivyo.

“Nimepokea taarifa ya vifo hivi kwa mshtuko mkubwa, nimehuzunishwa na kuondokewa na idadi hii kubwa ya watu, nampa pole Gregory Teu kwa kufikwa na msiba huu mkubwa, nawapa pole wanafamilia, ndugu na jamaa wote walioguswa na vifo hivi. Nawaombea marehemu wote wapumzishwe mahali pema na pia nawaombea majeruhi wote wanaopata matibabu huko nchini Uganda wapone haraka na kurejea nyumbani,” amesema Rais Magufuli.

Aidha, Rais Magufuli amewataka wanafamilia wote kuwa na moyo wasubira, uvumilivu katika kipindi hiki kigumu cha kuondokewa na wapendwa wao.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,270FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles