29.9 C
Dar es Salaam
Monday, December 4, 2023

Contact us: [email protected]

Madee: Tuzitumie fursa tunazopata

madeeNA CHRISTOPHER MSEKENA
NYOTA wa Bongo Fleva, Hamad Ally ‘Madee’, amewataka wasanii maarufu kutumia vizuri fursa zinazowazunguka
kama yeye alivyotumia jina lake kuanzisha kampuni ya ukodishaji magari inayoitwa Tiptop Connection Tour.
Akizungumzia biashara hiyo, Madee alisema mpango wa kuanzisha kampuni hiyo ulianza muda mrefu ila mwaka huu ameona afanye kweli kwani biashara hiyo inalipa.
“Ni kampuni ambayo inajihusisha na ukodishaji magari kwa ajili ya watu wote wa ndani na nje ya Dar es Salaam, hadi sasa tuna magari mapya saba aina ya Noah hiyo ni mipango yangu kwa mwaka huu,” alisema Madee.
Aliongeza kuwa wasanii wengi wamewekeza kwenye biashara za nguo lakini yeye ameamua kuwa tofauti nao kwa kuanzisha kampuni hiyo ya kukodisha magari.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
580,000SubscribersSubscribe

Latest Articles