Uwoya hapendi kuweka wazi mambo yake

0
1158

 

uwoyaNA THERESIA GASPER, DAR ES SALAAM

MSANII wa filamu za nchini, Irene Uwoya, amefunguka na kusema hapendi kuweka wazi mambo yake binafsi kama ilivyo wasanii wengine.

Msanii huyo alisema kuwa kuna baadhi ya wasanii ambao wanapenda kuweka kila kitu chake ambapo haina maana yoyote kwa jamii.

Akizungumza na MTANZANIA, msanii huyo alisema anapendelea kufanya mambo yake kwa siri na sio kuweka wazi kwenye mitandao ya kijamii kama wanavyofanya baadhi ya wasanii.

“Ukweli ni kwamba, sipendi kuweka mambo yangu hadharani au kutaja gharama ya vitu ninavyovifanya, napendelea mambo yangu kuyafanya yawe ya siri,” alisema Irene

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here