23.8 C
Dar es Salaam
Monday, September 25, 2023

Contact us: [email protected]

Mabango ya TAWA yavutia Watalii Sabasaba

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Mabango ya Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) yenye picha za Wanyamapori, Hifadhi za Magofu ya kale na vivutio mbalimbali vinavyopatikana katika maeneo yanayosimamiwa na shirika hilo yamekuwa vivutio vikubwa kwa watalii wanaotembelea Banda la TAWA katika maonyesho ya 46 ya Sabasaba jijini Dar es Salaam.

Ubunifu uliotumika katika kuyaandaa umekuwa sababu ya wananchi wengi wanaotembelea banda la TAWA kupenda kupiga picha (selfie) katika mabango hayo.

TAWA inaendelea kuwakaribisha wananchi wote katika banda lake lililo ndani ya banda la Wizara ya Maliasili na Utalii katika viwanja vya Mwl. Nyerere jijini Dar es Salaam.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,718FollowersFollow
574,000SubscribersSubscribe

Latest Articles