30.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Rita Kabati aongoza wenye ulemavu kumpongeza Rais Samia na kuhamasisha Sensa

Na Mwandishi Wetu, Iringa

Wananchi Mkoani Iringa wametakiwa kuacha kuwaficha watu wenye ulemavu katika zoezi la sensa ya watu na makazi linalotarajiwa kufanyika hapa nchini Agosti 23, mwaka huu.

Kauli hiyo imetolewa leo Jumamosi Julai 9, 2022 na Mbunge wa Viti maalumu Mkoa wa Iringa, Ritta Kabati ambaye pia ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Rita Kabati Trust Fund wakati wa kongamano la watu wenye ulemavu lililoasisiwa na Taasisi yake leo katika viwanja vya Garden Posta mkoani hapa.

Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Queen Sendiga akizungumza na hadhara iliyohudhuria katika Kongamano hilo alipokuwa akitoa hotuba yake kuzindua rasmi kongamano hilo lililofanyika leo Julai 9,2022 kwenye viwanja vya Posta katikati ya Mji wa Iringa. Sendiga ametumia jukwaa hilo kukemea vitendo vya ukatili wa kijinsia viivyokithiri katika mkoa huo na kuwataka wazazi wenye watoto wenye ulemavu kutowaficha katika zoezi la Sensa linalotarajia kufanyikaAgosti 23, mwaka huu.

Kabati amesema kuwa watu wenye ulamavu wana wajibu wa kushiriki katika zoezi la sensa kwa kuwa litaisaidia serikali kupata takwimu sahihi za watu hao ambazo zitasaidia kupata Fursa mbalimbali zilizopo katika serikali inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia suluhu Hassan ikiwemo Mikopo, fursa za elimu, ujasiriamali, kijamii na kisiasa.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Queen Sendiga ambaye alikuwa Mgeni Rasmi katika kongamano hilo la watu wenye ulemavu amesema kuwa kundi hilo lina wajibu wa kushiriki katika zoezi la sensa ya watu na makazi huku akiwataka wazazi wenye watoto au familia yenye watu wenye ulemavu kutokuwaficha katika zoezi hilo.

Sehemu ya Umati wa watu wenye ulemavu wakisikiliza Hotuba zilizokuwa zikitolewa na viongozi waliokuwa wakizungumza kwenye Kongamano hilo.

Awali akizungumzia kuhusu Umuhimu wa sensa ya watu na Makazi Mratibu wa zoezi hilo na Mtakwimu wa Halmshauri ya Manispaa ya Iringa, Raymond Nyanzwa amesema kuwa takwimu muhimu za watu wenye ulemavu zitaisaidia serikali kujua ni idadi kiasi gani ya kundi hilo inahitaji kutatuliwa changamoto zao.

Kwa upande wake Mjumbe wa halmashauri Kuu CCM Taifa, Theresia Mtewele amesema kuwa Chama cha Mapinduzi CCM kimejipanga kuhakikisha kinatoa elimu kupitia viongozi wao kuanzia ngazi ya Mtaa hadi kitaifa ili kuhakikisha watu wenye ulemavu wanashiriki katika zoezi la sensa ya mwaka huu ambayo ni ya sita toka Tanzania iungane na Zanzibar mwaka 1964.

Mwalimu wa Shule ya Msingi visiwi Mkoa wa Iringa ambaye ni mtaalamu wa Lugha ya alama, Mwl. Alikasuswe Mwandosya (kulia) akiwaongoza wanafunzi wake wenye ulemavu wa kusikia kutafasili hotuba mbalimbali zilizokuwa zinatolewa na wageni waliopo meza kuu akiwemo Mgeni rasmi Mhe. Queen sendiga (hayumo pichani) kwenye Kongamano hilo lililofanyika mkoani Irnga leo Julai 9,2022. PICHA ZOTE NA: HUGHES DUGILO

Zoezi la Sensa husadia Serikali kupata taarifa za msingi zitakazosaidia mchakato wa utekelezaji wa dira ya Maendeleo ya Mwaka 2025, Mageuzi ya masuala ya afya na jamii, pamoja na ufuatiliaji wa ajenda za maendeleo za kimataifa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles