24.1 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

Maandamano makubwa yatikisa mji wa Urusi

KHABAROVSK, URUSI

MAELFU ya waandamanaji wamemiminika katika mitaa ya mji wa Mashariki ya mbali ya Urusi wa Khabarovsk, wakipinga kukamatwa kwa gavana wa mkoa huo, kutokana na tuhuma za kuhusika katika mauaji. 

Vyombo vya habari vya ndani vimekadiria kuwa kiasi ya waandamanaji 50,000 wameshiriki maandamano  hayo yaliyofanyika jana. 

Maandamano hayo yamefanyika kila siku ndani ya wiki hii, ambapo mamia ya watu walikusanyika katikati ya mji, na kuashiria hasira kubwa juu ya kukamatwa kwa gavana na kutoridhika na sera za serikali ya Urusi. 

Sergei Furgal, gavana maarufu wa Khabarovsk alikamatwa wiki mbili zilizopita na kusafirishwa hadi Moscow na kuwekwa jela kwa muda wa miezi miwili. 

Anatuhumiwa kushiriki kwenye mauaji kadhaa ya wafanyabiashara kati ya mwaka 2004 na 2005 kabla ya kuanza safari yake ya kisiasa.

Wakati huo huo Ripoti mpya ya wizara ya ulinzi ya Marekani Pentagon, imeeleza kuwa Uturuki iliwatuma kiasi ya wapiganaji 3,500 hadi 3,800 wa Syria nchini Libya katika kipindi cha miezi miwili ya kwanza ya mwaka huu. 

Ripoti hiyo imetolewa wakati mgogoro katika taifa hilo lenye utajiri wa mafuta Libya, ukizidi kuongezeka katika vita vya mataifa ya kigeni nchini humo yanayoingiza silaha na wapiganaji katika taifa hilo. 

Jeshi la Marekani lina wasiwasi na ongezeko la ushawishi wa Urusi nchini Libya, ambako mamia ya wapiganaji wa kirusi wanaunga mkono kampeni ya kuutwaa mji mkuu wa Tripoli. 

Ripoti hiyo ya robo mwaka kuhusu operesheni za kukabiliana na ugaidi barani Afrika, inasema Uturuki iliwalipa na kutoa uraia kwa maelfu ya wapiganaji kuungana na wapiganaji wa serikali ya Tripoli dhidi ya vikosi vya kamanda Khalifa Haftar.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles