23.4 C
Dar es Salaam
Saturday, April 27, 2024

Contact us: [email protected]

Maalim Seif amaliza ziara Marekani

Seif_Sharif_HamadNa Mwandishi Wetu

KATIBU mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad, amemaliza ziara yake nchini Marekani na kuelekea Canada.

Maalim Seif alihitimisha ziara yake hiyo kwa mkutano wa hadhara ambapo alipata nafasi ya kuzungumza na Watanzania waishio nchini humo.

Katika mkutano huo, mwanasiasa huyo alisema kuwa lengo la ziara yake ni kuuelezea ulimwengu kuhusu kile kilichotokea Zanzibar kutokana na uchaguzi uliofanyika Oktoba 25 na mwelekeo wa demokrasia nchini Tanzania kwa ujumla.

Alisema ziara yake nchini Marekani imezaa matunda. “Sina budi kumshukuru Mwenyezimungu kuwa tumeeleweka na ziara yetu imezaa matunda,” alisema Maalim Seif ambaye alikua mgombea urais wa Zanzibar katika uchaguzi huo.

Akizungumzia zoezi la uchaguzi wa mwaka jana visiwani Zanzibar, Maalim Seif alisema uchaguzi huo ulihudhuriwa na waangalizi wa kimataifa na wa ndani.

“Waangalizi wote, wote kabisa, walikiri kuwa uchaguzi ulikuwa huru na wa haki. Ulikuwa uchaguzi bora kabisa kuliko chaguzi zote zilizotangulia Zanzibar,” alisistiza Maalim Seif

Alisema mchakato wa uchaguzi kuwa ulikwenda vizuri mpaka kufikia Oktoba 27, jumla ya majimbo 34 ya uchaguzi yalikuwa tayari yameshatangazwa na mengine tisa yakiwa yameshahakikiwa ikiwa bado kutangwazwa .

“Na kwa upande wa udiwani na uwakilishi, uchaguzi ulikuwa umeshakamilika na washindi kupewa shahada zao za ushindi.

“Kufika hapo tukashuhudiwa vituko vya Tume ya Uchaguzi hususan mwenyekiti wake”, alisema Maalim Seif,

Maalim Seif, alisema kitendo cha Mwenyekiti wa ZEC, Jecha Salim Jecha, cha kufuta uchaguzi huo kinakiuka sheria za uchaguzi.

Pamoja na hali hiyo, alisema alichukua hatua kadhaa ikiwemo za kujaribu kutatua mgogoro huo, ambapo moja ya hatua hizo muhimu ni kuwasiliana na Rais wa Zanzibar,  Dk. Ali Mohamed Shein, ambaye pia alikuwa mgombea wa urais.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles