25.3 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 29, 2022

Contact us: [email protected]

Lukuvi awapa madiwani Power Tiller

lukuviphotoNA RAYMOND MINJA IRINGA

MBUNGE wa Isiman ambaye Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi ametoa Power Tiller 15 kwa madiwani  wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa ajili ya kuwasaidia kutekeleza shughuli za maendeleo.

Pia ametoa  msaada  wa  mabati  2,000  kwa  ajili ya  kukamilisha  miradi  mbalimbali ya  maendeleo katika   jimbo hilo, vyote  vikiwa na thamani ya Sh milioni 100.4

Akizungumza na waandishi wa habari juzi,Katibu wa mbunge huyo,  Thom Malenga alisema  Lukuvi amewapa madiwani  mashine ikiwa ni sehemu ya kuwawezesha kuleta maendeleo.

Amewataka madiwani kuwatumika wananchi ipasavyo ili kumuunga mkono mbunge kwa kukuza uchumi wa kila kata na kulifanya jimbo la ismani kuwa na maendeleo ya haraka kwa kuwa madiwani  wapo karibu na wananchi .

Akizungumzia msaada wa mabati, Malenga  alisema  lengo la kuunga mkono kazi zilizofanywa na wananchi ya kusimamisha kuta katika miradi ya  ujenzi wa  shule ,nyumba  za walimu na  zahanati ambazo  zilikuwa  zikihitaji bati  ili kukamilisha ujenzi wao.

“Mbunge  amewaunga mkono   wananchi  kwa kazi  kubwa waliyoifanya ya  kusimamisha  kuta za  vyumba vya madarasa na zahanati na kwa ajili ya  kuwaunga mkono ameamua   kununulia  bati hizi ili iwe rahisi kukamilisha miradi hiyo ili wanachi wetu waweze kupata huduma muhimu kwa uharaka zaidi,”alisema.

Kwa upande wake,Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Iringa Vijijini, Khalfani Hassani alisema madiwani ndiyo wa kwanza kukutana na changamoto kabla ya kuwezeshwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
205,436FollowersFollow
558,000SubscribersSubscribe

Latest Articles