27.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

Vyuo vikuu bora vya Saud Arabia

chuo-kikuu-cha-king-abdulazizNa FARAJA MASINDE

SAUDI Arabia ni kati ya nchi ambazo mfumo wake wa elimu umekuwa wa kiwango cha juu kwenye ukanda huo mzima wa Mashariki ya Kati au Falme za Kiarabu kwa ujumla huku ikiwa ni miongoni mwa nchi zenye vyuo vikuu bora zaidi duniani.

Katika kulidhihirisha hilo vyuo saba kutoka nchini humo vimekuwa miongoni mwa vyuo bora duniani kwa mwaka 2016/17 kwa mujibu wa utafiti wa Shirika la QS, huku taifa hilo likishika nafasi ya 19 kati ya 100 katika mataifa ya Kiarabu yenye mfumo bora wa elimu.

Kama ilivyo kwa vyuo vya mataifa mbalimbali duniani, vyuo vya Saudi Arabia pia vimekuwa vikitoa elimu ya kiwango cha Shahada, Shahada ya Uzamili na Shahada ya Uzamivu.

Kuwapo kwa mazingira bora na upatikanaji wa mahitaji muhimu ni moja ya kigezo ambacho kimekuwa kikifanya vyuo vya taifa hilo kutamba kwenye tafiti mbalimbali za kimataifa.

Taifa hilo ambalo utajiri wake mkubwa unatokana na utajiri mkubwa wa mafuta ambapo huchangia utajiri wa taifa hilo kwa zaidi ya asilimia 20 kwa kipindi cha nusu karne.

Utajiri huo wa nishati ndio umesababisha kuimarika kwa huduma mbalimbali kama vile usafiri, biashara, utalii, elimu, teknolojia, usanifu majengo, utamaduni na vitu vingine vingi ambavyo vimekuwa ni kielelezo thabiti cha taifa hilo duniani.

Kustawi kwa nishati hiyo ndiko kulikofanya taifa hilo kuanza kutoa hata ufadhili wa kiwango cha juu kwa wanafunzi wanaosomea masuala ya nishati nchini humo.

Lakini kitu cha kuzingatia kama una ndoto ya kusoma nchini humo ni suala la dini kwani vyuo vikuu vingi vimekuwa vikizingatia kigezo cha dini.

Ambapo vimekuwa vikifuata misingi ya Uislamu utaratibu ambao umewekwa na Serikali.

Hivyo kama nia yako ni kusoma kwenye vyuo vikuu nchini humo hivi ndivyo vyuo bora vya unavyopaswa kuomba kujiunga.

 

Chuo Kikuu cha King Fahd

Hiki ni kati ya vyuo vikuu vyenye majina makubwa katika ukanda mzima wa Mashariki ya Kati ambapo kinashika nafasi ya 189 duniani.

Kilianzishwa rasmi mwaka 1963 na kinapatikana katika mji wa Dhahran ambao ni kituo kikuu cha mafuta nchini humo, kikiwa na uwezo wa kuchukua wanafunzi 7,000 huku wanafunzi wa kike wakiwa hawaruhusiwi kujiunga na chuo hicho.

Chuo hicho pia ni kati ya vyuo 50 duniani vinavyofanya vizuri kwenye sekta ya madini, huku kikiwa kwenye orodha ya vyuo bora 150 duniani kwenye nyanja ya utoaji wa taaluma ya uhandisi wa Kemia.

 

Chuo Kikuu cha King Saud

Chuo hiki kilianzishwa mwaka 1957, kinashika nafasi ya tatu ya ubora katika vyuo vikuu vya kiarabu kwa mwaka 2016 kati ya vyuo 227 duniani.

Kimekuwa kikitoa taaluma ya Uhandisi wa Sayansi, Uuguzi, Sayansi ya Kompyuta, Uhandisi wa Makenika Elimu na mafunzo ya ufundi.

Kina jumla ya wanafunzi 51,000 huku zaidi ya wanafunzi 11,000 wakitoka mataifa ya kigeni, pia chuo hiki kinachukua wanafunzi mchanganyiko.

 

Chuo Kikuu cha King Abdulaziz

Ni Moija ya vyuo bora nchini humo kikiwa nafasi moja nyuma ya kile cha Mfalme Saud katika utafiti wa mwaka 2016 kwenye vyuo vikuu vya mataifa ya kiarabu na cha 283 duniani.

Kilianzishwa mwaka 1967 kikiwa na zaidi ya wanafunzi 82,000 waliogawanyika kwenye matawi mbalimbali ambao ni wanawake na wanaume.

Chuo hiki kiko katika mji wa Jeddah, ambapo kilibuniwa na msanifu wa Kiingereza anayefahamika kama John Elliott. Kinatoa taaluma ya hesabu, Kemia, Sayansi na uhandisi wa makanika sanjari na taaluma za madawa.

Vyuo vikuu vingine bora nchini humo ni pamoja na Umm Al-qura, King Khalid, King Faisal , Al-imam Mohamed Ibn Saud Islamic , Alfaisal, Prince Sultan na Qassim.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles