24.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

LUKUVI AKABIDHI HATI 4,000 KWA WAKAZI KIMARA

Na ANASTAZIA MAGUHA (TURDACO)

-DAR ES SALAM

WAZIRI wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi,

Na ANASTAZIA MAGUHA (TURDACO)

-DAR ES SALAM

WAZIRI wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi, amekabidhi hatimiliki 88 kwa wakazi wa Kimara, Dar es Salaam kati ya 4,333 ambazo ziko kwenye hatua za mwisho katika mradi wa urasimishaji wa makazi holela.

Akikabidhi hatimiliki hizo jana, Waziri Lukuvi, alisema hati ni mtaji uliofufuliwa baada ya wakazi kuishi na kuendeleza maeneo yasiyopimwa, ambayo hutambulika kama mtaji mfu jambo ambalo hakuna mtu yeyote ambaye ngeweza kupata mkopo bila kutumia hati.

Alisema Serikali ya Awamu ya Tano ina dhamira ya dhati ya kurasimisha makazi nchi nzima ili kuongeza thamani ya ardhi au maeneo husika.

“Kwa hati hizi zilizotolewa takribani 4,333 tukisema kila nyumba ikopeshwe kwa kiwango cha chini cha shilingi milioni 10, kwa siku ya leo Kimara inapata mtaji wa karibu bilioni 40.5,” alisema Lukuvi.

Aliongeza kuwa maeneo yote ya miji ambayo hayajapimwa, yapimwe na halmashauri na manispaa zote nchini ili kuyaongezea thamani na kuondokana adha ya watu kujenga kwenye makazi holela.

Lukuvi pia alitoa onyo kali kwa matepeli wa ardhi kuacha vitendo hivyo mara moja kwani dawa yao ipo tayari.

Aliongeza kuwa na madalali uchwara wa ardhi waache tabia ya kuwaonea wanyonge na kusababisha mali zao ziuzwe kwa njia ya udanganyifu.

Kwa upande wake, Meya wa Manispaa ya Ubungo, Boniface Jacob, alimpongeza Waziri Lukuvi kuwa ni mtu anayejali maendeleo ya wananchi bila kujali vyama vyao wala itikadi zao.

Alisema waziri huyo anafuata nyayo za Rais Dk. John Magufuli ambaye anafanya maendeleo kwa Watanzania wote bila kujali vyama vyao.

Naye mkazi wa Kilungule, Kimara ambaye amekadhiwa hati, Prackson Lugazia, alisema hatua hiyo ya kupata hati ni jambo zuri na la maendeleo kwani ataweza kunufaika na fursa mbalimbali ikiwamo mikopo kupitia taasisi za fedha.

Utoaji wa hati hizo umefanyika kupitia Mpango wa Urasmishaji wa Makazi Holela katika Kata za Saranga na Kimara, Dar es Salaam na kusimamiwa na Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.

, amekabidhi hatimiliki 88 kwa wakazi wa Kimara, Dar es Salaam kati ya 4,333 ambazo ziko kwenye hatua za mwisho katika mradi wa urasimishaji wa makazi holela.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles