26.9 C
Dar es Salaam
Tuesday, May 21, 2024

Contact us: [email protected]

RUTO: WAKENYA TUKUBALI MATOKEO BILA FUJO

Mgombea mwenza wa Chama cha Jubilee, nchini Kenya, William Ruto amewataka Wakenya kukubali matokeo ya uchaguzi kwa amani bila kufanya fujo au vurugu.

Amesema hayo baada ya kumaliza kupiga kura mapema leo Agosti 8, katika uchaguzi mkuu unaofanyika nchini humo.

“Tukielekea kukamilisha kupiga kura tunataka Wakenya wajue ni wajibu wetu kama Wakenya kupiga kura, tusianzishe vurugu au fujo, tuko na nchi nyingi ambazo wameelekeza macho yao kwetu.

“Demoktrasia siyo fujo, ni kuamua kwa mapenzi yako vile unataka mambo yako yaendeshwe na kina nani.

“Kwa hiyo mimi nataka niwaambie ndugu zangu Wakenya tutekeleze hili na baada ya kupiga kura tuwe na subira na baadaye tulekeze nguvu zetu kwa mshindi, sote ni wakenya atakayeshinda ni Mkenya na usiposhinda safari hii utashinda wakati mwingine, yule aliyepata kura nyingi tumpatie nafasi baada ya miaka mitano tumpe nafasi mwingine tutakayemchagua,” amesema Ruto akiongea na vyombo vya habari.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles