24.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

Lugola: kutokuwa na kitambulisho cha taifa ni kosa

Felix Mwagara, Mara

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, amewataka wananchi wenye sifa yakupata vitambulisho vya taifa nchini kwenda  kujisajili katika ofisi za Mamlaka ya Vitambulisho hivyo (NIDA) katika wilaya wanazoishi kwani ni lazima kila Mtanzania awe nacho.

Lugola amesema kuna wananchi ambao hawakujitokeza wakati usajili ulipokua unafanyikakatika mitaa na vijiji vyao, na pia wapo ambao kipindi hicho walikuwa na miaka17 na kukosa sifa ya kujisali, lakini kwasasa wamefikisha miaka 18, naowanapaswa kufika ofisi za wilaya ili wapate huduma hiyo ya usajili.

Akizungumza na wananchi wa Mji wa Kibara, mkoani Mara, Lugola amesema zoezi la kujisajilisi la kupuuzwa kwa kuwa ni lazima kila mwananchi raia wa Tanzania awe na kitambulisho cha Taifa.

“Vitambulisho hivi ni muhimu kuwa navyo, nawaomba Watanzania msipuuze hili zoezi, na pia napenda kusisitiza kwa mara nyingine muelewe vizuri kuwa vitambulisho hivyo vitatolewa kwa Watanzania wenye sifa tu ambao watapita katika mchujo ili kuepusha kutoa kwa wasio raia,” amesema.

- Advertisement -
Previous article
Next article

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles