27.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]


Kesi ya ‘picha za ngono’ za Wema Sepetu kusikilizwa tena Januari 28, 2019

KULWA MZEE – DAR ES SALAAM 

Upande wa Jamhuri katika kesi inayomkabili msanii wa filamu nchini ambaye pia ni mrembo wa Tanzania mwaka 2006, Wema Sepetu umedai upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika.

Hayo yamedaiwa leo Decemba 12 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na Wakili wa Serikali, Mosia Kaima, wakati kesi hiyo ilipotajwa mbele ya Hakimu Mkazi, Maira Kasonde kwa ajili ya kutajwa.

Kaima aliiomba mahakama ipange tarehe nyingine ya kuitaja ili kuangalia kama upelelezi utakuwa umekamilika ama la.

Hakimu Masonde baada ya kusikiliza maelezo hayo aliiahirisha kesi hiyo hadi Januari 28 mwakani, itakapotajwa tena.

Katika kesi hiyo, Wema anadaiwa kuwa Oktoba 15, mwaka huu katika maeneo mbali mbali ya jiji la Dar es Salaam alichapisha video ya ngono na kusambaza katika mtandao wake wa kijamii wa Instagram.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles