Lugola aagiza vituo vya ukaguzi magari barabarani vipunguzwe

0
883

Pendo Fundisha, MbeyaWaziri Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, amemuagiza Inspekta Jenerali wa Polisi, Simon Sirro, kupunguza vituo vya ukaguzi wa magari visivyo na lazima ambavyo vimeonekana kutumiwa vibaya na askari wa usalama barabarani wasio waadilifu.

Lugola ameyasema hayo leo Jumatano Oktoba 3, wakati akizungumza na waandishi wa habari katika ziara yake Mjini Mbeya akitokea mkoani Rukwa.

Amesema vituo hivyo ambavyo vilivyowekwa baada ya kila hatua 20 kwa lengo la kudhibiti ajali, vimegeuzwa na kuwa fursa kwa baadhi ya askari.

“Askari wamekuwa wakiwaumiza wananchi, wanasimamisha magari kila kituo, vituo vipo kila zaidi ya hatua 20, halafu kazi kubwa ni kuomba na kupokea rushwa,” amesema Lugola.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here