27.5 C
Dar es Salaam
Sunday, December 3, 2023

Contact us: [email protected]

Lowassa kuanza ziara ya kuwashukuru wananchi

lowassa-1Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

ALIYEKUWA mgombea urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), chini ya mwamvuli wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), Edward Lowassa, anatarajia kufanya mkutano wa hadhara kesho jijini Tanga, ikiwa ni sehemu ya ziara ya kuwashukuru Watanzania waliompigia kura wakati wa uchaguzi mkuu.

Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari Dar es Salaam jana na Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Chadema, Tumaini Makene, ilisema katika ziara hiyo Lowassa ataambatana na viongozi wengine waandamizi wa Ukawa, ikiwa ni mwanzo wa ziara ya nchi nzima.

“Watawashukuru kwa namna walivyounga mkono upinzani na ajenda ya mabadiliko katika uchaguzi mkuu uliopita na wanavyoendelea kuweka matumaini yao kwa upinzani kuwa ndiyo nguzo imara wanayoweza kuitegemea kuwaletea mabadiliko ya kweli kwa ajili ya maendeleo yao na ustawi wa taifa kwa ujumla.

“Itakumbukwa mbali ya Watanzania kupiga kura za ushindi katika nafasi ya urais katika uchaguzi mkuu uliopita, wananchi waliwachagua wabunge wengi wa upinzani wanaotokana na Ukawa na kuongeza nguvu kubwa ndani ya Bunge, hususan kupitia Kambi ya Upinzani Bungeni,” ilisema taarifa hiyo.

Taarifa hiyo ilisema kuwa kambi rasmi ya upinzani bungeni itakuwa Serikali mbadala ya wananchi.

“Wameviamini vyama vyetu hivyo kusimamia na kuongoza halmashauri zipatazo 34 nchi nzima, ikiwa moja ya misingi imara katika kupigania mabadiliko ambayo Watanzania wanayataka,” inasema taarifa hiyo.

Taarifa hiyo ilifafanua kuwa wananchi wanastahili shukrani kwa imani hiyo ambayo ni ishara ya kuwa matumaini yao kwa miaka mingine mitano yatasimamiwa na kuongozwa na upinzani imara kupitia Ukawa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
579,000SubscribersSubscribe

Latest Articles