24.1 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Dhamana ya vigogo TRA Sh bilioni 7.8

Pg 2Na Patricia Kimelemeta, Dar es Salaam

MAHAKAMA Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam, imeridhia kutoa dhamana kwa watuhumiwa watatu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na kuwataka kila mmoja kutoa fedha taslimu Sh bilioni 2.6.

Akisoma uamuzi huo jana, Jaji Winfrida Koroso, aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni Tiagi Masamaki (56) ambaye ni Kamishna wa Forodha wa mamlaka hiyo, Burton Mponezya (51) na Habibu Mponezya (45) ambaye ni Meneja wa Kitengo cha Huduma kwa Wateja.

Alisema kabla ya kutoa dhamana hiyo, mahakama hiyo imepitia maelezo ya pande zote mbili ambazo ni upande wa washtakiwa na wa Serikali ili kuangalia kama watuhumiwa hao wana vigezo vya kupewa dhamana.

Jaji Koroso alisema baada ya kupitia maelezo hayo, mahakama iliridhia kuwapatia dhamana hiyo, huku ikiwataka kutimiza masharti sita ili waweze kukidhi vigezo.

Aliyataja masharti hayo kuwa ni kila mwombaji kulipa fedha taslimu Sh bilioni 2.6 au mali yenye thamani ya fedha hizo na kudhaminiwa na wadhamini wawili ambao ni wafanyakazi wa Serikali wenye bondi ya Sh 20 kila mmoja.

Alisema, kila mwombaji hatakiwi kusafiri bila ya kibali cha Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ambako kesi hiyo inaendeshwa, kuwasilisha vibali vya usafiri ikiwamo paspoti katika mahakama hiyo na kuripoti mahakamani hapo kila baada ya wiki mbili siku ya Jumatatu.

Alisema masharti mengine ni kila mwombaji ahakikishe taarifa zote alizowasilisha mahakamani hapo ziwe zimesainiwa kisheria na kukamilisha taratibu za dhamana ndani ya saa 24 ili waweze kukidhi vigezo vya dhamana hiyo.

Awali, Masamaki na wenzake walifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, wakituhumiwa kufanya makosa mawili ya uhujumu uchumi ambapo shtaka la kwanza ni kutoa makontena 329 katika Bandari ya Dar es Salaam bila ya kulipiwa kodi na kuisababishia Serikali hasara ya Sh bilioni 12.7.

Katika shtaka la kwanza, ilidaiwa mahakamani hapo kuwa tarehe tofauti kati ya Juni mosi na Novemba 17 mwaka huu, sehemu isiyojulikana ndani ya Jiji la Dar es Salaam, watuhumiwa hao kwa pamoja walikula njama ya kuidanganya Serikali kuwa Sh bilioni 12.7 zimetolewa kwa kutoa makontena 329 katika bandari kavu ya Azam baada ya kodi zote kutolewa.

Shtaka la pili, inadaiwa kuwa Juni mosi na Novemba 17, mwaka huu ndani ya Jiji la Dar es Salaam, walishindwa kutimiza majukumu yao kwa namna inavyotakiwa na kusababisha Serikali kupata hasara ya Sh bilioni 12.7.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles