22.2 C
Dar es Salaam
Thursday, August 11, 2022

Lowassa awasili Arusha

Mwandishi Wetu, Arusha

Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowassa, amewasili jijini Arusha akitokea Dar es Salaam na kulakiwa na viongozi na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), mkoani Arusha na Monduli mkoani Manyara akiwamo Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM, Wilaya ya Karatu, Daniel Awakii.

Lowassa aliwasili Uwanja wa Ndege wa Kisongo saa 6:20 mchana, akiambatana na mkewe mama Regina Lowassa, mtoto wake Robert na rafiki zake Maxon Chizii, aliyekuwa Katibu wa CCM Wilaya ya Babati, Edward Porokwa na Hamisi Mgeja.

Lowassa anaelekea wilayani Monduli ambako atapokewa rasmi na viongozi wa CCM akiwamo Katibu wa Itikadi na Uenezi, Humphrey Polepole.

Lowassa alitangaza kurejea rasmi CCM Machi Mosi mwaka huu na kupokewa na Mwenyekiti wa chama hicho Rais John Magufuli, Makamu Mwenyekiti, Philip Mangula, Katibu Mkuu, Dk. Bashiru Ally na viongozi na wanachama mbalimbali katika Makao Makuu ya chama hicho Lumumba jijini Dar es Salaam.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,415FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles