Vipodozi , mitandao ya kijamii vilivyompa utajiri wa kutupa Kylie

0
1152

KATIKATI ya mwezi Novemba mwaka jana, msichana mdogo wa Marekani kutoka familia maarufu, The Kardashian, Kylie Jenner, alifanya mambo makubwa baada ya kutembelea maduka ya kuuza bidhaa mbalimbali.

Kwa kipindi cha miaka mitatu, bidhaa zake za vipodozi zilizojulikana kama  Kylie Cosmetics, zilikuwa zinauzwa mtandaoni pekee, lakini akapatiwa mafunzo kuhusu maduka.

Uamuzi wa mdogo huyo wa kuzaliwa na mwanamitindo maarufu duniani, Kim Kardashian, kukubali kusaini mkataba wa usambazaji wa bidhaa zake kupitia duka la mitindo na urembo la Ulta, bidhaa za Kylie Cosmetics zilipanda bei ikiwemo lipstick ambazo zilitoka bei ya dola 29 hadi dola 1,000.

Kylie Jenner alitembelea duka hilo lililopo mtaa wa Richmond Avenue jijini Houston na kusalimiana na wateja, kusaini vitabu vya kumbukumbu na kuweka sahihi pamoja na kupiga picha na mashabiki wake.

Kwa mujibu wa takwimu za Oppenheimer, takribani wiki sita tangu kuwekwa kwenye duka la Ulta, Kylie Cosmetics iliuza bidhaa zenye thamani ya dola milioni 54.4 ikiwa ni rekodi ya kipekee dukani hapo.

“Niliweka kwenye maduka machache, kisha nikatangaza kupitia kurasa zangu za mitandao ya kijamii, nilifanya kitu ambacho mtu yeyote angelifanya, ilileta faida,” alisema Kylie Jenner.

Aingia kwenye orodha ya mabilionea wa Forbes

Kuuzwa kama njugu kwa bidhaa za urembo na mitindo za Kylie Cosmetics, kumemletea faida kwa asilimia 9 mwaka jana ambayo ni sawa na dola milioni 360. Kutokana na kasi ya kukua huko kwenye soko la urembo, jarida la biashara la Forbes liliitaja Kampuni ya Jenner kuwa na thamani ya dola milioni 900, ambazo zote anamiliki mwenyewe.

Thamani ya bidhaa za Jenner zimepanda kwa kasi na kuwa bilionea huku akiwa na miaka 21, ambapo thamani ya biashara yake inakadiriwa kuwa itafikisha kiasi cha dola bilioni 1.

Ni msichana mdogo ambaye amejiweka katika ngazi ya kuwa bilionea na kufika kuwa bilionea mwenye umri mdogo zaidi kuliko wote akiwemo Mark Zuckerberg, mwasisi wa mtandao wa Facebook (ambaye aliingia kwenye kundi la mabilionea akiwa na umri wa miaka 23 wakati alipotikisa kupitia mtandao wa Facebook).

“Sikutegemea kitu kama hicho, wala sikufikiria kama siku moja huko mbele nitakuwa bilionea. Lakini kutambuliwa thamani hiyo ni heshima na kitu kizuri. Ni nguvu ya mitandao ya kijamii,” alisema Jenner.

Uzuri wa bidhaa za Kylie Cosmetics, ambazo Jenner alianzisha mwaka 2015, zimemwingizia fedha nyingi mfukoni mwake.

Uwezo wake kwenye utajiri umetokana na kufanya kazi kwa saa 7 na saa 5 kwa muda wa ziada. Amefanya kazi kwenye kampuni binafsi ya Seed Beauty iliyoko Oxnard jijini California.

Biashara zake zinauzwa na kusimamiwa mtandaoni na Shopify.

Mama yake, Kris anasimamia upande wa fedha na mahusiano kwa umma. Upande wa masoko, matangazo mengi yanafanyika katika mitandao ya kijamii ambako Jenner ana wafuasi wengi.

Anatangaza bidhaa zake kupitia mitandao ya kijamii ya Snapchat, Instagram, Facebook na Twitter.

“Ni nguvu za mitandao ya kijamii. Nililazimika kufikia idadi kubwa kabla ya kuanza kufanya chochote.” anasema Jenner.

Wakati Kylie Cosmetics ilipozinduliwa, iliwafikia watu wengi kiasi kwamba oda zilikuwa nyingi kupitia mtandaoni kila baada ya dakika moja. Maduka ya Ulta yalijaza wateja na kujikuta yakiishiwa bidhaa ndani ya muda mfupi.

“Tuliuza bidhaa nyingi kuliko tulivyopanga na kutarajia,” anakiri Tara Simon, Makamu wa Rais wa Ulta.

Ulta na Jenner zimeungana na kufanya faida kubwa. Maduka ya Ulta yamewazidi kete washindani wao kama vile MAC Cosmetics Nyx Professional Makeup na Sephora.

Uchambuzi unaonesha kuwa Kylie Cosmetics wateja wake wakubwa ni vijana na watoto ambao huenda hawana vigezo vya kununua bidhaa kupitia mtandaoni. Vile vile wanauza ana kwa ana, huku wateja wakipata nafasi ya kukutana na Jenner moja kwa moja.

“Kuna wateja wanaofika hapa, wakitaka kumwona, kumgusa na kununua bidhaa huku wakiwa na nafasi ya kupiga naye picha.”

Maduka ya Ulta yanauza bidhaa kwa wananchi wa Marekani hususan tabaka la kati pamoja na kutegemea uwezo wa Jenner mwenyewe kuwasiliana na wateja takribani milioni 120 ambao ni wafuasi wake mtandaoni.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here