27 C
Dar es Salaam
Friday, May 27, 2022

Abdi Banda: Sijaitwa Taifa Stars sababu ni makocha

Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

BEKI wa Baroka FC ya Afrika Kusini, Mtanzania Abdi Banda amesema kutokuwa na kutokuwa na maelewano mazuri na makocha wawili wa timu ya Taifa, (Taifa Stars), ndiyo sababu kuu ya yeye kutokuitwa katika kikosi cha wachezaji 25 kilichotajwa hivi karibuni kwa ajili ya kuikabili timu ya taifa la Uganda (The Cranes) Machi 24 Uwanja wa Taifa Dar es Salaam.

Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Emmanuel Amunike, ametangaza majina hayo akiwajumuisha wachezaji wengi wanaocheza nje ya Tanzania lakini jina la Abdi Banda ambaye ni beki tumaini wa timu ya Baroka likikosekana, katika orodha ya majina hayo ya wachezaji watakaokutana na The Cranes Machi 24, mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Abdu Banda ameiambia Mtanzania Digital kuwa kuachwa kwake katika kikosi hicho kunatokana na ni kutokuwa na maelewano mazuri na makocha wote wa timu hiyo.

Amesema ugomvi wake na mmoja wa makocha hao ulianza alipokuwa akiichezea timu ya Coastal Union ya Tanga kabla ya kusajiliwa na Simba na chuki hizo zilisambaa hadi akakosanishwa na benchi lote la ufundi la timu ya Taifa.

 “Sipatani na makocha wote wa Taifa Satars kwa sasa nimeamua kupumzika kuchezea timu ya Taifa, nguvu zangu nimezihamishia katika klabu yangu ya Baroka pamoja na familia kwa ujumla,” amesema Banda.

Kocha Mkuu wa timu hiyo, Amonike amesema amechagua timu hiyo kutokana na kuonyesha kujali taifa na kuwa tayari kupigania Watanzania.

Majina ya wachezaji wa timu ya Taifa itakayoingia kambini na timu zao kwenye mabano ni makipa Metacha Mnata(Mbao), Suleiman Salula (Malindi FC-Zanzibar), mabeki  Vicent Philipo (Mbao FC) na Kennedy Wilson (Singida United).

Nyota wengine ni Kikosi makipa Aishi Manula,(Simba), Aron Kalambo (Tz Prisons) , viungo Feisal Salum, (Yanga) Mudathiri Yahya (Azam FC), Yahya Zayd (Ismail ya Misri) na Jonas Mkude (Simba).

Mabeki ni Hassan Kessy, (Nkana Rangers ya Zambia), Gadiel Michael, Kelvin Yondani, Andrew Vincent ‘Dante’ (Yanga), Ally Mtoni (Lipuli FC)  huku mawinga wakiwa Shiza Kichuya (ENPPI  Club ya Egpty) Simon Msuva (Difaa El Jadida ya Morocco) na Faridi Mussa (Tenerife ya  Spain)

Washambuliaji ni Shabani Chilunda (Tenerife ya Spain), Rashid Mandawa (BDF X1  ya Botswana) Mbwana Samatta (Genk Ubelgiji ) Thomas Ulimwengu (JS Saoura ya Algeria) na John Boko (Simba).

Stars inatarajia kuingia kambini Machi 17, mwaka huu kutokana na baadhi ya wachezaji kuwa katika michuano ya Ligi mbalimbali ndani na nje ya nchi.

Katika msimamo wa kundi L, nayeongoza ni  Uganda  yenye pointi  saba, ikifuatiwa na Tanzania yenye pointi tano sawa na Lesotho  iliyopo nafasi ya tatu, Cape Verde ya mwisho ina pointi nne.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
192,454FollowersFollow
541,000SubscribersSubscribe

Latest Articles