28.2 C
Dar es Salaam
Thursday, August 11, 2022

Kocha Simba amgomea Kagere, amkumbuka Kichuya

Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

BAADA ya baadhi ya timu ikiwemo Raja Casablanca ya Moroco na Zamaleck ya Misri kuonyesha nia ya kutaka sahini ya mshambuliaji hatari wa Simba, Meddie Kagere kwa kuonyesha nia ya kutoa zaidi ya Sh bilioni 1, uongozi wa timu hiyo umekataa ofa hiyo kwa sasa kwa sababu ya mechi zake za kimataifa.

Awali uongozi wa Raja Casablanca na Zamaleck ulikutana na wakala wa Kagere, Patrick Gakumba ukiwa umetenga dau la dola 450,000 kwa ajili ya kumsajili mchezaji huyo ambaye alijiunga na Simba msimu huu akitokea GorMahia ya Kenya.

Licha ya yote hayo Kocha Mkuu wa Simba, Patrick Aussems amewaambia uongozi wa klabu hiyo kwamba hayupo tayari kuona mchezaji wake muhimu akiondoka kama ilivyokuwa kwa Shiza Kichuya.

Amesem Simba inahitaji kufanya vizuri katika michuano ya kimataifa hasa kucheza robo fainali hali ambayo ni muhimu kuwatunza wachezaji wake.

“Kagere ni mtu muhimu sana katika kikosi changu, nimewambia uongozi sio muda sahihi wa kumuuza mchezaji,” amesema kocha huyo.

Hata hivyo taaruifa za ndani za timu hiyo zinadai kuwa timu nyingine nyingi zimetaka sahini ya mchezaji huyo lakini kocha huyo hataki kusikikia ofa ya timu yeyote kwa kipindi cha sasa.

“Kwa sasa haondoki mtu, lakini hapo baadae dirisha la usajili litakapofunguliwa na bodi tutakapokaa na kupitia ripoti ya kocha na kama kutakuwa na ofa kubwa kutoka kwa timu hizo kwa ajili ya Kagere tutazifikiria lakini si kwa sasa kocha hataki,” kilieleza chanzo hicho.

Kagere hadi jana, Machi 8 ameshapachika mabao 12 ikiwemo michezo ya ligi kuu na Ligi ya mabingwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,455FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles