26.8 C
Dar es Salaam
Saturday, September 7, 2024

Contact us: [email protected]

Lipumba asikitishwa makubaliano Serikali, TCD kutupwa kapuni

lipumbaNA GRACE SHITUNDU, DAR ES SALAAM
CHAMA cha Wananchi (CUF) kimesema makubaliano baina ya vyama vya siasa na serikali ya kuboresha baadhi vifungu katika Katiba ya Mwaka 1977 ili vitumike katika Uchaguzi Mkuu mwaka huu vimetupwa kapuni huku wananchi wakiwa gizani na hatima ya uandikishaji katika Daftari ya Kudumu la Wapigakura.
Hayo yalisemwa na Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba jana alipokuwa akifungua kikao cha siku mbili cha Baraza la Uongozi wa chama hicho kitakachojadili mambo mbalimbali ikiwamo umarishaji wa ushirikiano wa vyama vinavyounda Umoja wa Katiba Tanzania (UKAWA).
Alisema katika kikao kilichofanyika kati ya Rais Jakaya Kikwete na Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD) kinachoundwa na vyama vyenye wabunge ambavyo ni CCM, Chadema, NCCR-Mageuzi, CUF, TLP, UDP na UPDP inayowakilisha vyama visivyo wa wabunge, kilichofanyika Ikulu ndogo Dodoma Septemba mwaka jana walikubaliana kufanyiwa marekebisha baadhi ya vifungu lakini havijafanyiwa kazi yoyote hadi sasa.
“Tulipokutana na Rais katika kikao cha Septemba mwaka jana ambacho kilikuwa ni cha pili tulikubaliana Serikali ipeleke muswada bungeni ili katika katiba ya sasa viwepo vifungu muhimu vinne.
Vifungu hivyo ni pamoja na kuwa na Tume Huru ya Uchaguzi, Rais kushinda kwa asilimia zaidi ya 50, kuwa na mgombea binafsi na matokeo ya urais yaweze kuhojiwa mahakamani,” alisema Profesa Lipumba.
Alisema pamoja na makubaliano hayo serikali iliendelea na mchakato wa kutafuta katiba mpya ambako katika kuelekea kura ya maoni wamekwama na kusimamisha upigaji wa kura hiyo iliyokua ifanyike Aprili 30 mwaka huu. Hata hivyo hakuna dalili ya kufanyika marekebisho hayo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles