22.8 C
Dar es Salaam
Wednesday, May 22, 2024

Contact us: [email protected]

Christian Bella: Belle 9 hana nyota

Belle-9Na Festo Polea
MWANAMUZIKI Christian Bella ‘King of melody’, amesema kwamba msanii wa bongo fleva, Ablenego Damian ‘Belle 9’, amekosa nyota ya kung’aa ingawa ana uwezo mkubwa wa kuimba kwa kutumia sauti yake.
Christian Bella alisema hayo katika kipindi cha ‘Mboni Show’. Alisema kati ya wasanii watatu wanaomvutia kwa kujua kuzitumia sauti zao, Belle 9 ni mmoja wao.
Aliwataja wasanii wengine kuwa ni Ali Kiba na Diamond.
“Nisiwe mnafiki, Diamond hana sauti nzuri kama Ali Kiba katika kuimba na Ali Kiba nimeshawahi kufanya naye kazi kwa kuimba ‘Live’ sauti yake ni ile ile, ni msanii mwenye uwezo mkubwa wa kuimba ‘live’, lakini Diamond ni mjanja wa kuichezea sauti yake na anafanikiwa kutangaza nchi kimataifa, lazima apongezwe kwa hili,’’ alifafanua Bella.
Bella aliongeza kwa kumtaka Ali Kiba kutojisahau muda mrefu, huku akimshauri kutoa nyimbo bila kuhofia lolote, kwa kuwa uwezo wake ni mkubwa na mashabiki wanataka awe anatoa nyimbo mapema.
“Lakini licha ya wawili hawa kufanya vizuri, bado sielewi kwa rafiki yangu Belle 9 ana nyimbo kali na sauti yake inakubalika sana, lakini sijui tatizo ni nyota au vipi, napenda sana kazi zake, ni staa kwangu,’’ alijieleza Bella.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles