24.2 C
Dar es Salaam
Sunday, May 19, 2024

Contact us: [email protected]

Wema: Kumuimba msichana uliyeachana naye ni ushamba

wemaNA RHOBI CHACHA
STAA wa filamu za kibongo, Wema Sepetu ‘Beautiful Onyinye’, amesema ni ushamba kwa wasanii wa muziki kuwatungia nyimbo za majungu wasichana wanaoachana nao kimapenzi.
Wema amesema wasanii wengi wa muziki wamekuwa na tabia ya kishamba ya kutunga nyimbo zenye maneno ya kuudhi, wakiwalenga waliokuwa wapenzi wao.
“Ni ushamba wa mapenzi, haiwezekani mlikuwa mnafurahia wote mapenzi yenu, lakini mkiachana anakutungia nyimbo za kukuponda, hakuna neno la kuzungumzia hilo zaidi ya kuita ushamba kwa wasanii wa aina hiyo,’’ alisema Wema.
Hata hivyo, kwa mujibu wa chanzo chetu cha ndani kutoka studio moja kubwa ya kurekodi muziki nchini, kuna wimbo wa wasanii wawili waliowahi kuimba pamoja na wimbo wao ukawa gumzo kwa mashabiki wa muziki huo, ambao wanamalizia kurekodi wimbo unaodaiwa unamzungumzia mrembo huyo wa Tanzania mwaka 2006.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles