Maya: Nami nazeeka bila kupata mtoto

0
1624

NA RHOBI CHACHA
BAADA ya mwigizaji Wema Sepetu kuweka wazi juu ya masikitiko yake ya kutopata mtoto licha ya kumtafuta kwa muda mrefu, mwigizaji mwingine wa Bongo Movie, Mayasa Mrisho ‘Maya’ naye ameibuka na kudai kwamba anazeeka bila kupata mtoto.
Maya alisema wasanii wenzake wana watoto na wengine wajawazito, lakini yeye bado hajabarikiwa kupata mtoto, jambo linalompa hofu ya kuzeeka bila mtoto.
“Nazeeka bila mtoto wa kumzaa, hapa namuomba Mungu aniwezeshe na kunifungulia uzazi niweze kupata motto, maana umri unakwenda, nitazeeka bila ya kuwa na mtoto jamani,’’ alisikitika Maya.
Kutokana na kauli hiyo, Maya anakuwa mwigizaji wa pili kuweka wazi ya moyoni mwake ya kutokuwa na mtoto na nguvu zao wamezielekeza katika maombi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here