29.8 C
Dar es Salaam
Sunday, September 15, 2024

Contact us: [email protected]

Lil Wayne aitukana Cash Money

Lil Wayne
Lil Wayne

NEW YORK, MAREKANI

BAADA ya bosi wa Kundi la Cash Money, Birdman kushindwa kulipa fedha kiasi cha Dola milioni 51 kwa msanii wake Lil Wayne, nyota huyo wa muziki ameamua kutunga wimbo wa kulitukana kundi hilo.

Lil Wayne anamdai bosi huyo kutokana na makubaliano ya kazi zao za muziki, lakini inadaiwa hadi sasa Birdman ameshindwa kulipa deni hilo, hivyo Lil Wayne akaamua kuandika wimbo unaowashambulia wasanii wote waliopo kwenye kundi hilo akiwemo bosi wao.

Kupitia ziara yake ya ‘Lil Weezyana Festival’, ambayo inaendelea New Orleans, msanii huyo mwishoni mwa wiki iliyopita alipanda jukwaani na kuutambulisha wimbo wake mpya ambao ulikuwa unawatukana wasanii hao na bosi wao.

“Kabla sijaanza kuimba naomba niongee maneno matatu, awali nilikuwa Cash Money lakini kwa sasa sipo tena huko kutokana na uongozi wao kuwa mbovu, kwa sasa nimeamua kufanya kazi mwenyewe,” alisema Lil Wayne.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles