23.1 C
Dar es Salaam
Tuesday, September 10, 2024

Contact us: [email protected]

Rihanna, Drake siyo siri tena

rs_1024x759-160506144130-1024-drake-rihanna-all-star-halftime-show-2011

NEW YORK, MAREKANI

BAADA ya kumalizika kwa Tuzo za MTV Video Music Awards mwishoni mwa wiki iliyopita, rapa Drake na Rihanna wameanza kuonekana wakiwa pamoja mara kwa mara.

Hiyo ni wazi kwamba wawili hao kwa sasa ni wapenzi hasa kutokana na kauli ya Drake katika tuzo hizo ambapo alipanda jukwaani na kuweka wazi kuwa alianza kumpenda Rihanna tangu akiwa na umri wa miaka 22, mwaka 2008.

Drake alidai kuwa katika wasichana ambao anawapenda kwenye maisha yake ni pamoja na Rihanna kwa kuwa ni mtu wake wa karibu, lakini baada ya kumalizika kwa tuzo hizo inadaiwa  waliondoka pamoja na asubuhi yake walionekana wakitoka kwenye hoteli inayoelezwa walipumzika humo usiku kucha.

Hata hivyo siyo mara ya kwanza kwa wawili hao kuonekana wakiwa pamoja na inadaiwa kwamba uhusiano wao ulianza mwaka 2010 baada ya Rihanna kutoa wimbo wake wa ‘What is My Name’  aliomshirikisha Drake.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles