20.9 C
Dar es Salaam
Saturday, June 15, 2024

Contact us: [email protected]

Mambo 7 muhimu kwa mwajiriwa

Depositphotos_9305586_m

Na ATHUMANI MOHAMED,

WATU wengi wanapokuwa mashuleni au vyuoni husoma kwa bidii kwa lengo la kupata ajira serikalini au taasisi mbalimbali mara baada ya kuhitimu masomo yao.

Siyo makosa kuwa na malengo hayo, maana akili za wengi zilishajikita huko baada ya kuaminishwa hivyo vizazi kwa vizazi. Ajira siyo jambo baya; wengi wameweza kupiga hatua kutokana na ajira zao.

Lakini hata hivyo, inaelezwa kuwa mwajiriwa kama asipokuwa makini, yupo kwenye hatari kubwa ya kufa masikini. Haina maana kwamba ajira ni mbaya, lakini ikiwa mwajiriwa hatakuwa makini na hesabu zake, atakuja kushtukia umri umekwenda na hakuna alichofanya.

Maisha ni kuchagua. Wapo waliochagua kuwa wakulima, wengine wameamua kufanya biashara huku wengine wakiwa waajiriwa sehemu mbalimbali.

Somo hili ni muhimu sana kwako wewe mwajiriwa ili uweze kufanikiwa ukiwa kwenye ajira yako. Ndugu zangu, hakuna anayependa kustaafu kazi akiwa hana kitu kwenye akaunti yake. Mambo haya muhimu yatakusaidia sana.

  1. USIGAWE FEDHA HOVYO

Baadhi ya watu wakishapata ajira, mishahara yao ikitoka huwa na kazi ya kuzigawa. Wapo watu ambao mishahara ikishaingia mikononi mwao ni kukimbilia baa.

Atakesha na kushinda tena baa siku inayofuata akitoa ofa kwa watu wanaomfahamu. Ndugu zangu, hakuna unachofanya huko, utasaga lami miaka na miaka na hutaona mafanikio yako kwa mchezo wako wa matumizi ya ovyo.

Heshimu fedha. Kuna wengine mishahara yao huwa mali ya ndugu. Kila mwezi kazi yake ni kutuma fedha kijijini. Sijasema ni vibaya kutuma fedha kwa ndugu au wazazi ambao wana uhitaji na wamekuwa msaada mkubwa kwa mhusika, lakini siyo iwe ndiyo desturi.

Wapo ndugu huko vijijini kwa kujua ratiba ya mshahara wa ndugu yake mjini, basi kila zikifika tarehe za mshahara atatengeneza tatizo ili atumiwe fedha, kuwa makini.

Hata hivyo, ni vizuri zaidi kusaidia watu wa muhimu na wenye uhitaji wa kweli, mfano wazazi, wadogo zako na ndugu wengine wa karibu.

Unaweza kudhani mshahara ni wa uhakika na wa kila mwezi kwa hiyo uuchezee uwezavyo lakini kumbe unaharibu mustakabali wako wa maisha yako ya baadaye. Heshimu mshahara wako.

Kuwa na hesabu. Mfano unalipwa 600,000 kwa mwezi. Kanuni za mafanikio zinaeleza kuwa unapaswa kuweka akiba ya nusu ya mshahara wako (50%), kisha robo iwe ya matumizi yako ya mwezi unaofuata na robo uweke kwa dharura zitakazojitokeza.

Kumbuka dharura ni pamoja na kusaidia ndugu nk. Usijichanganye, kuwa na huruma yenye kiasi. Utakuja kushtuka unamaliza miaka kazini na huna cha maana ulichofanya.

  1. BUNI VYANZO VIPYA

Hata kama wewe ni bosi ofisini kwako, lazima uwe mbunifu na ujue utawezaje kupandisha kipato chako nje ya ajira yako. Hakuna mtu aliyewahi kufanikiwa kutokana na mshahara wake wa mwezi.

Kama kuna mtu wa namna hiyo basi siyo mwadilifu kazini na atakuwa anatumia vibaya madaraka yake. Wapo waajiriwa wengi waliofanikiwa, lakini ukiwauliza watakuambia siri ni kuwa na vyanzo vingine vya mapato.

Namna bora ya kubuni kitu cha kufanya ni kuangalia zaidi kipaji chako. Kamwe usifanye kitu kinachoshabihiana au kama unachofanya kwa mwajiri wako ili kuepuka mgongano wa kimasilahi.

Buni biashara au kazi utakayofanya katika muda wako wa ziada au mara baada ya kutoka kazini. Ukiwa na vyanzo vingine vya mapato, ni wazi kuwa utakuwa umeongeza kipato chako.

Wiki ijayo tutaendelea na mada yetu, usikose tafadhali.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles