26.2 C
Dar es Salaam
Thursday, June 1, 2023

Contact us: [email protected]

LHRC Yalaani Mauaji Ya Kikatili Mkoani Tabora

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Kituo cha Sheria na Haki za Bindam(LHRC)kimelaani matukio ya ukiukaji wa haki za binadamu unaofanywa na Askari wa Mamlaka Usimamizi ya Wanyamapori Tanzania (TAWA) huku hatua zikishindwa kuchukuliwa na mamlaka husika kwa wale waliohusika kufanya ukiuaji huo.

Mkurugenzi Uwezeshaji na Uwajibikaji Joyce Komanya akizungumza na waandishi kuhusiana na ukiukaji wa Haki za Binadamu.

Mauaji yamekuwa yakifanywa kwenye hifadhi lakini kukiwa na mamlaka kujichukulia hukumu ya kuua watu licha kuwepo kwa vyombo vya kutoa haki dhidi ya wanaokiuka sharia zilizowekwa katika hifadhi hizo nchini.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo hicho, Anna Henga kufuatia na tukio lililotokea hivi karibuni mkoani Tabora kufuatia TAWA kwa kushirikiana na Askari Polisi wa Kituo cha Polisi cha Igagala kuchoma nyumba kwa amri ya mkuu wa Wilaya ya Kaliua aliyekuwepo katika kipindi cha hivi karibuni.

Henga amesema kuwa katika nyumba iliyochomwa ulikuwa na mtoto wa miaka minne (4) Nyanzobhe Mwandu ambaye alifariki kwa mauaji ya kikatili hayo bila ya kuwa na hatia hiyo na kuuawa kwa katika hifadhi ni jambo lisilokubalika wa nchi inayofuata misingi ya Haki na Utawala bora.

Mkurugenzi Mtendaji huyo amesema vitendo hivyo vimekuwepo kwa muda mrefu dhidi ya ukiuaji wa haki za binadamu katika hifadhi za maliasili pamoja na kutofauta taratibu za kuundosha watu katika maeneo hayo ili kufanya maisha ya wanyama yawe katika starehe.

“Wanannchi wanaokuwepo na sharia zimewekwa wakiwa kaika maeneo hayo kuwa wamekiuka taratibu za kuwaondosha zipo na kuweza kuwafikisha mahakamani lakini suala la kuua watu wakiwa katika maeneo hayo halipo,” amesema Henga.

Amesema aliyetoa amri kwa sasa hayupo lakini suala la jinai haliwezi likaisha hata miaka 1,000.

Kifo cha mtoto huyo zinasema kwamba serikali kupitia Mamlaka za Hifadhi ya Taifa ilitenga eneo la Hifadhi katika Kijiji cha Ngitiri amabyo inazunguka na Vijiji kadhaa Wananchi ambao mashamba yao yanapakana na hifadhi hivyo walitakiwa waondoke ili kupisha ardhi iliyotengwa.

Taarifa zinasema kuwa mwezi Januarie mwaka 2021 wananchi waliruhusiwa kulima kwa makubaliano ya kwamba baada msimu wa mavuno kuisha walitakiwa kuondoka katika eneo la mavuno.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,225FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles