22.2 C
Dar es Salaam
Monday, October 14, 2024

Contact us: [email protected]

Dk. Mwinyi: Zanzibar inaunga mkono MSD kujengga kiwanda

Unguja, Zanzibar

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi amesema kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inaunga mkono azma ya Bohari ya Dawa (MSD) ya kutaka kujenga kiwanda cha dawa hapa Zanzibar.

Rais Dk. Mwinyi ametoa pongezi hizo leo Jumatatu Juni 21, 2021 Ikulu jjini Zanzibar wakati alipokutana na kufanya mazungumzo na Meja Jenerali Saali Mhidze Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD) akiwa amefuatana na ujumbe wake.

Katika maelezo yake Rais Dk. Mwinyi alieleza kwamba azma ya Bohari ya Dawa (MSD), ya kuja kuekeza viwanda vya dawa hapa Zanzibar itasaidia kwa kiasi kikubwa hasa katika wakati huu wa janga la COVID 19 ambapo upatikanaji wa dawa na vifaa tiba kutoka nje sio mzuri.

Rais Dk. Mwinyi alitoa pongezi kwa hatua zilizoanza kuchukuliwa na (MSD), za kutaka kuanzisha viwanda hapa Zanzibar ambazo zitapelekea kutotegemea sana dawa kutoka nje ya nchi hali ambayo athari yake imeweza kuonekana hasa katika kipindi hichi cha maradhi ya COVID 19 duniani.

Aidha, Rais Dk. Mwinyi alisema kuwa hatua hiyo ya kuanzisha viwanda inaungwa mkono na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar hasa ikizingatiwa kwamba tayari imeshatenga maeneo maalum ya viwanda na Serikali iko tayari kutoa ushirikiano wake.

Rais Dk. Mwinyi alieleza ipo haja ya kuonekana kwamba bidhaa zinazozalishwa Zanzibar nazo ni sehemu za biashara kutoka Tanzania na kuondoa vikwazo vya kibiashara ambavyo hapo siku za nyuma vilikuwepo na kusababisha biashara kati ya sehemu mbili za Muungano kuwa ngumu.

Pia, alieleza azma ya Zanzibar ya kufanya bidhaa zozote zinazozalishwa hapa nchini kuagizwa nje ya nchi huku akieleza jinsi Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inavyoiungana na Bohari ya Dawa (MSD) ya kuanzisha viwanda vya ndani hapa hapa nchini.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles