29.7 C
Dar es Salaam
Friday, October 4, 2024

Contact us: [email protected]

RC Malima awataka Ma-DC wapya kutotumia madaraka vibaya

Na Amina Omary, Tanga

Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Adam Malima amewataka wakuu wa Wilaya wapya walioteuliwa na Rais Samia Suluhu Juni 19, 2021 kwenda kufanyakazi na kuacha kutumia madaraka vibaya kwa kuwaweka ndani watu kwa uonevu.

Malima aliyasema hayo leo Jumatagtu Juni 21, 2021 wakati alipowaapisha wakuu wa wilaya ambapo amewataka kutambua nafasi waliyopewa ni kubwa hivyo waende wakawatumikie wananchi katika kuhamasisha maendeleo.

“Msiende kuitumia sheria ya masaa 48 vibaya bali itumike kwa haki na sio kwa uonevu kwani nyie ndio walinzi wa amani katika maeneo yenu,” amesema Malima.

Aidha, amewataka wakaweke mikakati ya kuinua sekta ya kilimo kwani sehemu kubwa ya wananchi wa Tanga wanategemea kilimo kama sehemu yao ya fursa za kiuchumi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles