22.7 C
Dar es Salaam
Sunday, June 4, 2023

Contact us: [email protected]

LADY JAYDEE, MWANA-FA JUKWAA MOJA USIKU WA ANAWEZA

Na Bethsheba Wambura, Dar es Salaam

Msanii mkongwe wa muziki wa kizazi kipya nchini (Bongo Fleva) Judith Wambura maarufu Lady Jaydee, ametambulisha msanii mwenzake Hamis Mwinjuma maarufu MwanaFA kama ndugu yake wa karibu.

Hii ni mara ya kwanza kupanda jukwaa moja tangu wawili hao kurudisha ukaribu wao baada ya kutokuwa katika maelewano kwa muda mrefu.

Lady Jaydee alifanya tamasha alilolipa jina la ‘Anaweza’ lililofanyika katika Ukumbi wa Bwalo la Maofisa wa Polisi Oysterbay, jijini Dar es Salaam usiku wa kuamkia leo huku akisindikizwa na wasanii mbalimbali Mwana FA.

Wasanii wengine waliokuwepo katika tamasha hilo ni mkali wa miondoko ya RnB Ben Pol, Alawi Junior, Nikki Mbishi, na wakongwe Domo Kaya na Bushoke.

Jaydee amewahi kufanya matamasha kadhaa likiwamo la Naamka Tena ambalo alilifanya baada ya kuwa kimya kwa muda mrefu na hili la Anaweza ambalo limepewa jina la wimbo wake mpya aliofanya na Msanii wa Reggae kutoka Jamaica, Luciano.

“Anaweza concert imekuja baada ya wimbo wangu na Luciano kutoka jamaica ambao nimeuachia hivi karibuni na hii ni kuonesha kuwa naweza kusimama peke yangu hata baada ya kupita katika mambo mengi yanayokatisha tamaa na kuvunja moyo,” amesema Jaydee.

Awali, tamasha hilo lilitangazwa kufanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip kabla ya kuhamishiwa ukumbi huo wa maofisa wa polisi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,283FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles