29.4 C
Dar es Salaam
Sunday, October 13, 2024

Contact us: [email protected]

MTULIA, DK. MOLLEL KUREJEA BUNGENI UPYA

Na Mwandishi Wetu

Wabunge wateule wawili wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), waliochaguliwa katika uchaguzi mdogo uliofanyika hivi karibuni, Maulid Mtulia (Kinondoni) na Dk. Godwin Mollel (Siha), wanatarajia kuapishwa kesho.

Wabunge hao ambao awali walikuwa wabunge kabla ya kujiuzulu na kuhamia CCM, wakati huo Dk. Mollel akiwa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) huku Mtulia akitokea Chama cha Wananchi (CUF).

Kwa mujibu wa taarifa ya Ofisi ya Bunge Kitengo cha Habari, Elimu na Mawasiliano, wabunge hao wateule wataapishwa katika Mkutano wa 11 wa Bunge utakaoanza kesho Jumanne Aprili 3, Mjini Dodoma ambapo pamoja na mambo mengine mkutano huo utakuwa ni mahususi kwa ajili ya mijadala na kupitisha Bajeti ya Serikali na kujadili hotuba ya hali ya uchumi wa taifa itakayowasilishwa Bungeni na Waziri wa Fedha na Mipango.

Aidha, Bunge litajadili utekelezaji wa bajeti za wizara zote kwa mwaka wa fedha 2017/18 na makadirio ya matumizi ya Serikali kwa mwaka huo wa fedha. 

Wakati huo huo, Bunge litafanya uchaguzi wa wenyeviti watatu wa Bunge kutokana na wenyeviti waliopo kumaliza muda wao kwa mujibu wa kanuni za kudumu za Bunge.

“Vilevile katika mkutano huu wa Bunge, Miswada ya Sheria miwili itawasilishwa ambayo ni Muswada wa Sheria ya Fedha za Matumizi wa Mwaka 2018 (The Appropriation Bill, 2018) na  Muswada wa Sheria ya Fedha wa Mwaka 2018 (The Finance Bill, 2018).

“Katika mkutano huu jumla ya maswali ya kawaida 515 yanatarajiwa kuulizwa na kujibiwa, aidha, kwa mujibu wa Kanuni ya 38 (1) ya Kanuni za Kudumu za Bunge wastani wa maswali 72 ya papo kwa papo kwa Waziri Mkuu yataulizwa na kujibiwa kwa siku za Alhamisi,” imesema taarifa hiyo. 

Pamoja na mambo mengine, Bunge pia litajadili na kupitisha Azimio la Kuridhia Makubaliano ya Paris kuhusu Kuboresha Utekelezaji wa Mkataba wa Mabadiliko ya Tabia Nchi.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles