La Kwetu Concert waomba msaada

0
953

FABIAN (1)NA GEORGE KAYALA

WAANDAAJI wa tamasha la La Kwetu Concert Family 2016 wameiomba Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Wizara ya Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, kusaidia tamasha la kupinga mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi, linalotarajiwa kufanyika katika mikoa ya Kanda ya Ziwa.

Mkurugenzi Mtendaji wa tamasha hilo, Fabian Fanuel, alisema tamasha hilo lina tija na umuhimu mkubwa kwa jamii, lakini ili lifanikiwe kama lilivyopangwa, serikali kupitia wizara hizo mbili ni budi zisaidie.

“Tamasha hilo litakalofanyika Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza Juni mwaka huu, limelenga kuibua waimbaji wa muziki wa injili wanaochipukia pamoja na kupinga mauaji ya albino,’’ alieleza Fabian.

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here