24.2 C
Dar es Salaam
Monday, May 27, 2024

Contact us: [email protected]

Mkwasa: Tusiwalaumu Chad kwa kujitoa Afcon

CHARLES BONIFACE MKWASANA SUZANA MAKORONGO (RCT)

KOCHA Mkuu wa timu ya Taifa ‘Taifa Stars’, Charles Boniface Mkwasa, amesema kitendo cha Chad kujitoa kwenye mbio za kusaka tiketi ya kushiriki Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika mwakani si suala la kuwalaumu kwani inatokea kama nchi ikiwa haipati ushirikiano wala mchango wowote kutoka kwenye shirikisho au Serikali.

Chad ilitarajiwa kucheza juzi na ‘Taifa Stars’, lakini ilijitoa kutokana na ukata walionao hali iliyopelekea kuiweka Taifa Stars iliyo kundi G kwenye mazingira magumu kwa kubaki na pointi moja baada ya mechi za Chad kufutwa kama kanuni za Shirikisho la Soka Afrika (CAF) zinavyosema.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Mkwasa alisema Tanzania imekua kama ina bahati mbaya kwani timu ilikua ikijipa maandalizi ya kutosha kwa ajili ya  kuingia kushiriki Afcon bila vikwazo, lakini sasa imetokea Chad kujitoa bila sababu za msingi na ilibidi wajitoe kabla hawajapangiwa nao kuliko walivyofanya.

“Kama Tanzania kujitoa tulitakiwa tujitoe mwaka 2014, lakini hatukukata tamaa tulijipa nafasi ya kujipanga na kuongea vizuri na Serikali kusaidia timu, Chad hawakutakiwa kukata tamaa hata hawajaangalia uzalendo, wangekaa kuzungumza na Serikali yao hata kama haiipi kipaumbele michezo,” alisema Mkwasa.

Alisema kwa upande wake yeye na  timu yake suala la Chad kujitoa ni changamoto kwao, Tanzania  ingejitoa ingekua ni jambo la aibu kwa nchi na ukizingatia Serikali ipo kwa ajili ya kusaidia timu.

“Hili ni funzo kwetu, tuangalie ili tujue wapi walikosea ili na sisi tusijekufanya mambo kama hayo, wanadai walikosa wadhamini, mambo haya yapo cha muhimu ni kujitahidi yasije kutokea kama hayo yaliyowakuta wenzetu japo wamepewa adhabu hiyo si suluhu ya kutatua tatizo, dawa ni kuondosha tatizo lisijirudie na sio kuwataka watoe faini,” alisema.

Taifa Stars kwa sasa inatarajia kucheza na Misri mchezo utakaochezwa Juni 4 mwaka huu.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles