24 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

Kuku choma Festival kurindima kesho Msasani Beach Club

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

LILE Tamasha la Kuku choma litafanyika kesho Desemba 10, 2022 Msasani Beach Club jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Guru Planet Limited, Nixon Martin amesema tamasha litaanza asubuhi hadi usiku ambako wajasiriamali na wadau mbalimbali watahidhuria tukio hilo muhimu kwa maendeleo ya kiuchumi.

Martin amesema tamasha hilo litakuwa na matukio kama michezo ya baharini, wasanii wa kudance, kuvuta kamba, utoaji wa zawadi kwa watakaoweza kushinda ubunifu wa biashara hasa ya ufugaji wa Kuku ambao watapatiwa zawadi.

Katika tamasha hilo wamewaalika viongozi mbalimbali kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi na watendaji wengine kutoka wizara hiyo.

Alisema tamasha hilo litajikita kwenye uelimishaji kuhusu ufugaji ambako wataalam wataeleza taratibu na changamoto huku tukio lingine ni kuunganisha vipaji mbalimbali ambako pia michezo mbalimbali itakuwepo kama kuwashindanisha Kuku wa Simba na Yanga, stand up comedy.

Naye Ofisa Masoko wa Guru Planet, Paul Michael alisema katika tamasha hilo kutakuwa na viingilio vitatu, Sh 10,000 ambacho mwingiaji atapewa kuku robo, Sh 30,000 Kuku nusu na vinywaji huku Sh 50,000 kuku mzima, chipsi na vinywaji na kiingilio kingine ni Sh 100,000 mteja atapatiwa kuku mzima, mchemsho, supu na vinywaji.

Aidha, Michael amesema wamevialika vyuo vikuu saba vya jijini Dar es Salaam ambavyo ni Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE), Chuo cha Mwalim Nyerere, Chuo Kikuu Kampala (KIU), Chuo cha Fedha (IFM) na Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT).

Mhasibu wa Kampuni hiyo, Halima Waziri wamejipanga kuwasaidia vijana kuondokana na tatizo la ajira.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles