23.2 C
Dar es Salaam
Friday, June 9, 2023

Contact us: [email protected]

KUBENEA ASAFIRISHWA, KUHOJIWA DODOMA LEO

Mbunge wa Ubungo, Saed Kubenea (Chadema), amesafirishwa kuelekea Dodoma chini ya ulinzi wa polisi tayari kwa kuhojiwa na Kamati ya Bunge ya Maadili, Haki na Madaraka ya Bunge.

Kubenea amesafirishwa kwa ndege leo Jumatano Septemba 20, saa moja asubuhi baada ya polisi kujiridhisha kuwa afya yake si njema usafiri kwa barabara.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa ameiambia Mtanzania Digital kuwa Mbunge huyo alikuwa na hati ya kukamatwa kutoka Jeshi la Polisi mkoani Dodoma, iliyokuwa inamtaka afikishwe huko jana.

“Kutokana na afya yake jana tulishindwa kumsafirisha kwa gari ikabidi tufanye taratibu za usafiri wa ndege leo, nafikiri tayari atakuwa ameshasafiri maana ilipangwa aondoke saa moja asubuhi,” amesema Kamanda Mambosasa.

Mbunge huyo anahojiwa na kamati hiyo kutokana na agizo la Spika wa Bunge, Job Ndugai aliyezitaka kamati hiyo na ile ya Ulinzi na Usalama kumhoji mbunge huyo kwa kauli yake aliyoitoa katika Kanisa la Ufufuo na Uzima wiki iliyopita kuwa Spika ni mwongo kwani ametaja idadi chache ya risasi alizoshambuliwa Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu, aliyeko nchini Kenya kwa matibabu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,351FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles