29.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, September 28, 2021

KUBENEA AMTAKA KABUDI KULIELEZA BUNGE MAZUNGUMZO YA MAKINIKIA

Mbunge wa Ubungo Saed Kubenea (Chadema)

Maregesi Paul, Dodoma            |      


Mbunge wa Ubungo Saed Kubenea (Chadema), amemtaka Waziri wa Katiba na Sheria, Profesa Palamagamba Kabudi alieleze bunge juu ya mazungumzo kuhusu mchanga wa makinikia yalikofikia.

Amesema pamoja na kwamba Waziri wa Madini, Angellah Kairuki hakugusia suala hilo, katika kitabu cha bajeti ya wizara hiyo kuna haja Profesa Kabudi kulieleza bunge juu ya mchanga huo kwa sababu wananchi wanata kujua kinachoendelea.

Kubenea ametoa hoja hiyo bungeni leo alipokuwa akichangia bajeti ya wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2018/19.

“Pamoja na hayo, tunaitaka serikali iliwezeshe Shirika la Madini Tanzania (Stamico) ili liweze kufanya kazi kwa mafanikio zaidi kwa kuwa lina wajibu mkubwa katika kusimamia sekta ya madini nchini,” amesema Kubenea.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
158,609FollowersFollow
519,000SubscribersSubscribe

Latest Articles