26.2 C
Dar es Salaam
Monday, October 3, 2022

ASSAD: MAJESHI YA MAREKANI YAONDOKE SYRIA

DAMASCUS, SYRIA


RAIS Bashar al Assad, amesema Marekani inapaswa kujifunza kutokana na mzozo wa Irak na kuyaondoa majeshi yake kutoka Syria.

Katika mahojiano na Kituo cha Televisheni cha Urusi Leo, Assad amesema Serikali yake imeanza kufungua milango kwa mazungumzo na waasi na ikishindikana watayakomboa maeneo yote kwa nguvu.

Aliwataja kuwa ni pamoja na wapiganaji wa Syrian Democratic Forces (SDF) wanaoungwa mkono na Marekani, SDF wanaodhibiti theluthi moja ya Syria hasa maeneo ya kaskazini na mashariki mwa Syria ambako majeshi ya Marekani yamepiga kambi.

Rais huyo amesema mazungumzo ndiyo njia ya kwanza watakayotumia kuafikiana na kundi hilo la Kikurdi na iwapo hilo litashindikana, basi watalazimika kuyakomboa maeneo yanayodhibitiwa na SDF kwa kutumia nguvu.

Assad ametolea mfano wa Irak, akisema majeshi ya Marekani yaliivamia na kuingia humo bila ya kuwa na msingi wowote kisheria na sasa nchi hiyo imesalia kuwa katika mzozo.

Alisema watu hawatakubali wageni kuingilia nchi za kanda hiyo ya Mashariki ya Kati.

Alipoulizwa na kituo hicho kuhusu mtazamo wa Rais wa Marekani, Donald Trump kuwa yeye ni ‘mnyama’, Assad alisema kile unachokisema kumhusu mtu mwingine ndivyo ulivyo.

Trump alimwita Assad mnyama baada ya shambulizi linalodaiwa kuwa la silaha za sumu katika eneo la Douma Aprili, mwaka huu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
202,573FollowersFollow
554,000SubscribersSubscribe

Latest Articles