24.8 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

Korea Kaskazini yasema haina mpango kuzungumza na Marekani

PYONGYANG, KOREA KASKAZINI 

KOREA Kaskazini imesema haina mpango wa kuendelea na mazungumzo baina yake na Marekani hivi karibuni. 

Mazungumzo hayo ni yale yanayolenga kuitaka Korea ya kaskazini iachane na mpango wake wa silaha za nyuklia. 

Akizungumza kupitia shirika la habari la taifa la Korea Kaskazini, Naibu wa kwanza wa Waziri wa Mambo ya nje wa nchi hiyo, Choe Son Hui alisema jana kuwa, nchi yake haioni uhitaji wowote wa kukutana na Marekani.

Choe ameyasema hayo wakati alipokuwa akijibu minong’ono kuwa mkutano mwingine kati ya Rais wa Marekani Donald Trump na Kiongozi wa Korea ya Kaskazini Kim Jong Un, utafanyika kabla ya Uchaguzi Mkuu wa Marekani wa mwezi Novemba mwaka huu.

Rais wa Korea Kusini, Moon Jae alipendekezwa tena kuwa mpatanishi katika mazungumzo hayo. 

Kwa mujibu wa maofisa wake, wakati wa mkutano kwa njia ya video uliofanyika Jumanne iliyopita, Moon Jae alisema kuwa anataka kufanya kila liwezekanalo kuwakutanisha viongozi hao wa Marekani na Korea Kaskazini kabla ya uchaguzi wa Novemba.

Kwa upande wake, mshauri wa zamani wa masuala ya usalama wa kitaifa wa Marekani John Bolton, naye pia  alisema Trump atakutana na Kim, muda mfupi kabla ya uchaguzi iwapo tu anaamini kuwa hilo litasaidia katika harakati zake za kutaka kuchaguliwa tena kutetea kiti chake.

Choe Son Hui amenukuliwa akisema “Marekani itakuwa imekosea sana kama inadhani mambo ya mazungumzo yatakuwa na mashiko kwetu”.

Korea Kaskazini inakabiliwa na vikwazo vikali vya kimataifa kutokana na mpango wake wa nyuklia. 

Mazungumzo ya nyuklia kati ya Marekani na Korea Kaskazini hayajaendelea tangu mkutano kati ya Trump na Kim nchini Vietnam mwezi Februari mwaka 2016.

Korea ya Kaskazini imesema mara kadhaa kuwa haina nia ya kuanza tena mazungumzo mapya hadi pale Marekani itakapoleta mapendekezo mapya.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles