23.9 C
Dar es Salaam
Monday, September 20, 2021

Mauaji ya Jamal Khashoggi: Uturuki yaanzisha kesi dhidi ya raia 20 wa Saudia bila wao kuhudhuria

RIYADH, SAUDIA 

RAIA 20 wa Saudia wamefunguliwa kesi bila wao kuhudhuria nchini Uturuki kutokana na mauaji ya mwandishi maarufu, Jamal Khashoggi  mwaka 2018.

Khashoggi aliyekuwa mkosoaji mkubwa wa mwanamfalme Mohammed Bin Salman, aliuawa na kundi moja la mawakala wa Saudia ndani ya ubalozi wa Saudia uliopo mjini Instanbul nchini Uturuki.

Washukiwa ni pamoja na washauri wawili wa mwanamfalme huyo wanaokataa kuhusika. 

Saudia ambayo ilikataa ombi la Uturuki kuwapeleka nchini humo wahusika , iliwahukumu watu wanane mwaka uliopita kuhusu mauaji hayo.

Watano kati yao walihukumiwa kifo kwa kushiriki moja kwa moja na mauaji hayo huku watatu wengine wakihukumiwa kifungo jela kwa kuficha mauaji hayo.

Kesi iliyokuwa ikiendelea nchini Saudia ilipingwa na mjumbe maalum katika umoja wa mataifa Agness Callamard , ambaye alisema Khashoggi alikua mwathiriwa wa mauaji yaliopangwa kimakusudi ambapo serikali ya Saudia inahusika.

Mchumba wa Khashoggi ambaye ni raia wa Uturuki, Hatice Cengiz, ni mmojwapo wa wale waliotoa ushahidi wao wakati wa ufunguzi wa kesi hiyo.

Baadaye aliwaambia waandishi waliojikusanya nje ya mlango wa mahakama hiyo kwamba alihisi mchakato wote unamdhoofisha kiroho na kisaikolojia.

Cengiz alisema ana matumaini na mfumo wa mahakama na kutangaza kwamba : Mpango wetu wa kutafuta haki utaendelea nchini Uturuki pamoja na maeneo mengine.

Hatice aliwaambia waandishi kwamba wana matumaini na mahakama ya Uturuki

Shahidi mwengine aliyetoa ushahidi wake alikuwa Zeki Demir raia wa Uturuki aliefanya kazi kama mtu wa mkono katika ubalozi wa Saudia.

Demir aliiambia mahakama kwamba aliitwa katika nyumba ya mkurugenzi wa ubalozi huo siku ambayo Khashoggi alitoweka na kuambiwa kuwasha oveni inayotumika kuchoma nyama.

”Kulikuwa na takriban watu watano au sita waliokuwepo” , alisema.

Kulikuwa na hofu…Ilikuwa kana kwamba walitaka niondoke haraka iwezekanvyo”. Demir aliongezea alirudi katika nyumba hiyo siku chache baadaye na kugundua kwamba rangi iliyokuwa katika oveni hiyo ilikuwa imetolewa.

Callamard, mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa ambaye pia alikuwa katika kesi hiyo , alisema: “Hatukuhamisha kesi ya mauaji ya Jamal kwasababu iwapo kesi hiyo ingefanyika nchini Saudia isingepatiwa uaminifu na uhalali.” 

“Hapa kwa mara ya kwanza, tuna waliohusika wakishtakiwa na kuna idadi kubwa ya wale walioruhusu uhalifu kufanyika,” aliongezea.

Kesi hiyo itasikilizwa tena Novemba 24

Mwandishi wa BBC anasema hakuna  hata mmoja miongoni mwa washukiwa hao wa Saudia walioripoti mahakamani.

Anasema hakuna hata mmoja ambaye huenda akasafirishwa kwa lazima kutoka Saudia hadi Uturuki ili kukabiliwa mahakamani , na Saudia tayari ishafanya kesi yake ambayo ilishutumiwa kwa kutokamilika.

Lakini kwa mjumbe maaluma wa UN , kwa mchumba wa mwandishi alieuawa na kwa marafiki zake wa karibu na ndugu zake huu ndio wakati wa kutoa ukweli wote.

Ukweli ni kwamba maofisa wa ujasusi wa Uturuki waligundua kwamba mauaji hayo yalifanyika katika ubalozi wa Saudia nchini Uturuki , hivyo basi Uturuki inamiliki kanda za sauti kuhusu muda wa mwisho wa mwandishi huyo ambaye alishindwa nguvu na kuuawa. 

Mwandishi huyo anasema kuna masuala ya kisiasa hapa pia.

Uturuki na Saudia ni mahasimu wakuu. Lakini wale wanaoshiriki katika kesi hiyo wanaamini inatoa fursa mpya ya kutoa ushahidi mpya na mbaya zaidi.

ALIVYOUAWA

Mwandishi huyo aliyekuwa na umri wa miaka 59 , ambaye alienda mafichoni nchini Marekani mwaka 2017, alionekana mara ya mwisho akiingia ubalozi wa Saudia  Oktoba 2, 2018 ili kuchukua stakhabadhi ambazo alihitaji kumuoa Cengiz.

Baada ya kusikiliza kanda za sauti kuhusu mazungumzo yaliyokuwa yakiendelea katika ubalozi huo yaliyopatikana na majasusi wa Uturuki, Callamard alibaini kwamba Khashoggi aliuawa kinyama siku hiyo.

Serikali ya Saudia ilisema mwandishi huyo aliuawa katika operesheni mbaya iliofanyika na mawakala wa kundi fulani.

Upande wa mashtaka wa Saudia ulisema kwamba mauaji hayo yaliagizwa na kiongozi wa kundi moja la majadiliano lililotumwa Istanbul kumchukua Khashoggi na kumrudisha nyumbani kwa njia ya kumshawishi ama iwapo hiyo ingefeli angelazimishwa.

Upande huo wa mashtaka ulitamatisha kwa kusema kwamba Khashoggi alilazimishwa baada ya kukabiliana na mawakala hao ambapo alidungwa sindano iliyokuwa na dawa nyingi, na kufariki

Mwili wake baadaye ulikatwa vipande vipande na kupatiwa mshiriki mmoja wa Saudi nje ya ubalozi huo. Mabaki hayo hayakupatikana.

Upande wa mashtaka wa Uturuki ulisema kwamba Khashoggi alizuiwa kupumua muda tu alipoingia katika ubalozi huo na kwamba mwili wake uliharibiwa.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
156,961FollowersFollow
518,000SubscribersSubscribe

Latest Articles