26.3 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 30, 2021

Kocha Yanga ataka mabao

Theresia Gasper – Dar es Salaam

KOCHA Mkuu wa Yanga, Luc Eymael, amesema licha ya kupata pointi tatu katika mechi zao bado anahitaji ushindi mnono zaidi kwa kufunga mabao mengi.

Yanga juzi iliendeleza wimbi la ushindi baada ya kuinyuka Mtibwa Sugar bao 1-0 katika mchezo uliochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Akizungumza baada ya mchezo huo, Eymael alisema wachezaji wake walicheza kwa kujituma lakini walipoteza nafasi nyingi za kufunga mabao.

“Tunashinda lakini ule sio ushindi ninaoutaka kwani nahitaji  mabao mengi zaidi, kuna kipindi Patrick Sibomana alikosa nafasi ya wazi kabisa ya kufunga, hivyo nahitaji kuendelea kufanya vizuri zaidi kwenye mechi zetu zinazofuata,” alisema kocha huyo.

Aliongeza kwa kusema, katika mchezo huo wachezaji wake walionekana kuchezewa vibaya ila mwamuzi hakuwaonyesha kadi za njano.

Upande wake Kocha Mkuu wa Mtibwa Sugar, Zuberi Katwila alisema walipambana ila bahati haikuwa upande wao na kufanya wapoteze pointi tatu ugenini.

“Nimeona mapungufu yaliyojitokeza hivyo tunaenda kuyafanyia kazi kabla hatujaendelea na mchezo mwingine tuliopanga kuvuna pointu tatu muhimu,” alisema.

Alisema wana mechi ngumu dhidi ya Ruvu Shooting hivyo umakini unahitajika zaidi kwa kuwa wakifanya makosa tena yanaweza kuwagharimu.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
167,509FollowersFollow
526,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles