25.2 C
Dar es Salaam
Monday, November 29, 2021

Azam FC waiota nafasi ya kwanza VPL

Theresia Gasper – Dar es Salaam

BAADA ya timu ya Azam FC kupata sare ya bao 1-1, juzi dhidi ya Mbeya City, Kocha msaidizi Iddy Nassor ‘Cheche’, amesema wataendelea kupambana kwa lengo la kuipigania nafasi ya kwanza katika msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Katika mchezo huo dhidi ya Mbeya City uliochezwa Uwanja wa Samora, Iringa timu hiyo haikuweza kutamba ugenini.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Cheche alisema mchezo ulikuwa na ushindani mkubwa lakini hawakukata tamaa hadi dakika 90 na kufanikiwa kusawazisha.

“Tumelazimisha sare ya bao 1-1 dhidi ya Mbeya City tukiwa ugenini, lakini malengo yetu yalikuwa ni kupata pointi tatu muhimu, ila tutaendelea kupambana ili tuweze kupanda hadi nafasi ya kwanza,” alisema.

Aliongeza kwa kusema, wanashukuru kumaliza mzunguko wa kwanza wakiwa nafasi ya pili katika msimamo hivyo wataendelea kuwa makini zaidi kwa kila mechi watakayocheza mzunguko wa pili.

Cheche alisema wanarejea nyumbani kuendelea na maandalizi kwa michezo mingine iliyo mbele yao kwani kwa sasa kila mmoja anahitaji ushindi.

Kocha huyo aliwataka mashabiki wa Azam waendelee kuwapa sapoti katika mechi zao ili wachezaji wawe na morali na kuendelea kupata matokeo mazuri.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
167,301FollowersFollow
526,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles