23.9 C
Dar es Salaam
Wednesday, July 24, 2024

Contact us: [email protected]

KNCU kunufaika na masoko ya Afrika Kusini na Ulaya

Safina Sarwatt, Kilimanjaro

Chama Kikuu cha Ushirika mkoani Kilimanjaro (KNCU) kimeanza kukusanya kahawa zaidi ya tani 150 kutoka kwa vyama vya ushirika mkoani humo baada ya kupata masoko ya uhakika Afrika Kusini na Ulaya.

Kahawa hizo nikutoka vyama mbalimbali ambavyo ni vyama shirika vya KNCU,kahawa hizo zitauzwa katika masoko ya bara la Ulaya, na Afrika kusini ambao tayari kuna masoko ya uhakika na kwa bei nzuri.

Akizungumza kwenye wiki ya Chakula Kaimu Meneja wa KNCU, Wilbert Lyimo amesema KNCU kupitia kitengo cha kahawa imeendelea kuwahamasisha wakulima wa vyama vya msingi vya ushirika kulima kahawa zisizotumia kemikali za viwandani “organic” kutokana na kuwa soko na bei nzuri.

“Kahawa za organic zina bei nzuri ambapo kilo moja inauzwa zaidi ya Sh 10,000 na soko lake ni la uhakika tofauti na kahawa ambazo siyo organic ni Sh 7,000 kwa kilo moja, hivyo tunaendelea kuwashauri wakulima kulima kahawa bora za organic kwani uzalishaji wake hautumii gharama kubwa,” amesema.

Lyimo amesema KNCU imeanza shughuli za ukusanyaji wa kahawa na kufanya biashara za kahawa nje nchi na tayari wamekusanya kahawa tani 150, ambazo zimehifadhiwa katika ghala za TCCCO.

Amesema KNCU imepata fedha za mikopo kutoka benki ya ushirika mkoani Kilimanjaro KCBL kwa ajili ya kununua kahawa kutoka kwa wakulima

Amesema mikakati ya chama hicho nikurudisha KNCU katika hadhi yake,na kwamba tayari wako katika mchakato wa kufanya uchaguzi wa viongozi wa bodi.

“Tupo katika mchakato wa kufanya uchaguzi wa viongozi lengo nikuwapata viongozi bora wenye uwezo na wadhilifu watakao weza kusimama vyama ushirika.

“Nafasi tano wajumbe wa bodi kulingana katiba ya KNCU ambao ni wajumbe tatu,mwenyekiti na makamu wenyekiti,tunasubiri mraji apange tarehe ya uchaguzi kutokana na kwamba ipo katika mamlaka yake ya kiuongozi,”amesema.

Mkulima wa kahawa katika kata ya Kindi, Geofrey Mallya alisema KNCU kwa sasa inatakiwa kuongeza wigo wa ununuaji wa kahawa kama ilivyokuwa miaka ya nyuma ili kuzuia wakulima kutotorosha kahawa nje ya nchi.

Amesema KNCU wanatakiwa kununua kahawa kwa bei nzuri kama ilivyokuwa zamani jambo ambalo pia litahamasisha wakulima wengi kulima zao hilo ambapo kwa siku za karibuni linaonekana kudorora kutokana na kukosa bei nzuri.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles