29.9 C
Dar es Salaam
Monday, March 4, 2024

Contact us: [email protected]

Mabondia JWTZ wajitosa Usiku wa Mwana Ukome

Na Winfrida Mtoi, Mtanzania Digital

MABONDIA wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Ismail Galiatano na George Bonabucha wanatarajiwa  kuwa miongoni mwa wataopanda  ulingoni Oktoba 30, mwaka huu katika pambano la ‘Dar Boxing Derby lililpewa jina la Usiku wa Mwana Ukome.

Katika usiku huo ambao mapambano makubwa yatakuwa kati Francis Miyeyusho na Adam Kipenda, Idd Pialali  akizichapa dhidi ya  Ramadhan Shauri kwenye Uwanja wa Kinesi, Dar es Salaam.

Kwa upande wa Galiatano atapigana na Allan Kamote, wakati Bonabucha atazichapa Haji Juma wote wakitokea Tanga.

Akizungumzia pambano hilo, Galiatano amesema mashabiki wake watarajie mchezo mzuri  na hana shaka na mpinzani wake kutokana na mazoezi anayofanya.

“Nimejiandaa vyema, naamini yoyote atakuja atafurahia kwa sababu nitamchezesha mpinzani wangu vile ninavyotaka mimi,” ametamba Galiatano.

Naye Bonabucha amesema mpinzani wake ajiandae kupata kichapo  ikiwezekana atamaliza mchezo mapema kwa K.O.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
583,000SubscribersSubscribe

Latest Articles